The chat will start when you send the first message.
1Naomi akamwambia mkwewe: Mwanangu, hainipasi kukutafutia mahali pa kutulia patakapokufaa?[#Ruti 1:9.]
2Tena Boazi siye ndugu yetu? ni yule, ambaye ulikuwa na vijakazi wake. Tazama, usiku wa leo Boazi anayapura mawele pake pa kupuria.
3Nenda koga na kujipaka mafuta, kisha vaa nguo zako nzuri, uende kushukia hapo pa kupuria, lakini uangalie, usijulikane kwake yule mtu, mpaka atakapokwisha kula na kunywa!
4Akienda kulala, upajue, atakapolala. Kisha uingie, uifunue miguu yake, upate kulala nawe; ndipo, atakapokuambia la kufanya wewe.
5Akamjibu: Yote, uliyoniambia, nitayafanya.
6Akashukia hapo pa kupuria, akayafanya yote, mkwewe aliyomwagiza.
7Boazi akala, akanywa, moyo wake ukachangamka, kisha akaenda kulala nyuma ya chungu la miganda. Ndipo, alipokwenda hapo polepole, akaifunua miguu yake, akalala naye.
8Ilipokuwa usiku wa manane, yule mtu akakupuka usingizini, akajiinua, mara akamwona mwanamke aliyelala miguuni pake.
9Akamwuliza: Wewe nani? Akasema: Mimi ni kijakazi wako Ruti; nawe umtandazie kijakazi wako pembe la blanketi lako! Kwani wewe ndiwe mwingiliaji.[#5 Mose 25:5; Ez. 16:8.]
10Akamjibu: Na ubarikiwe na Bwana, mwanangu! Haya mema yako ya nyuma, uliyoyafanya, yanayapita ya kwanza kwa wema, usipowafuata vijana, kama ni maskini au kama ni wenye mali.[#Ruti 2:11.]
11Sasa mwanangu, usiogope! Yote, utakayoniambia, nitakufanyizia; kwani watu wangu wote waliomo malangoni mwangu wanakujua wewe kuwa mwanamke mwema sana.
12Sasa hii ni kweli, mimi ni mwingiliaji; lakini yuko mwingiliaji mwenzangu anayepaswa nanyi kuliko mimi.
13Usiku huu lala hapa! Kesho asubuhi itajulikana: akiwa anataka kukuingilia, basi, ni vema, na akuingilie! Lakini akiwa hataki kukuingilia, mimi nitakuingilia kwa hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima! Lala tu, mpaka kuche!
14Akalala miguuni pake, hata kulipokucha; akaamka hapo, mtu asipoweza bado kumtambua mwenzake; Boazi akamwambia: Isijulikane, ya kuwa mwanamke amefika hapa pa kupuria!
15Akasema: Lete kanga, uliyojifunika, uishike! Akaishika, akampimia pishi sita za mawele, akamtwika, kisha akaenda zake mjini.
16Ruti alipoingia kwa mkwewe, akamwuliza: Habari gani, wewe mwanangu? Akamsimulia yote, yule mtu aliyomfanyizia.
17Kisha akasema: Amenipa hizi pishi sita za mawele, kwani aliniambia: Usiende mikono mitupu kwa mkweo.
18Naye akamwambia: Kaa tu, mwanangu, mpaka utakapolijua hilo jambo, litakavyoendelea. Kwani yule mtu hatatulia, asipolimaliza leo hilo jambo.