The chat will start when you send the first message.
1Boazi akapanda kwenda langoni pa mji, akakaa huko. Mara yule mwingiliaji, Boazi aliyemtaja, akapita; ndipo, alipomwambia: Njoo, wewe bwana fulani, ukae hapa! Akaacha kwenda, akaja kukaa.
2Kisha akachukua watu kumi walio wazee wa mjini, akawaambia: Kaeni hapa! Nao wakakaa.
3Akamwambia huyo mwingiliaji: Fungu la shamba lililokuwa lake ndugu yetu Elimeleki, Naomi aliyerudi kutoka kwenye mbuga za Moabu anataka kuliuza.
4Nami nimesema, niyaeleze masikioni pako kwamba: Linunue machoni pao wanaokaa hapa napo machoni pao wazee wa ukoo wangu! Kama unataka kulikomboa, haya! Likomboe! Kama hutaki kulikomboa, niambie, nijue! Kwani kuliko wewe hakuna awezaye kulikomboa, mimi mwenyewe ni nyuma yako. Akasema: Basi, mimi nitalikomboa.[#3 Mose 25:25.]
5Boazi akamwambia: Siku, utakapolinunua hilo shamba mkononi mwa Naomi na mwa Ruti wa Moabu, umempata naye huyo mke wake yeye aliyekufa, ulikalishe jina lake aliyekufa katika fungu lake.[#5 Mose 25:5-6.]
6Ndipo, yule mwingiliaji aliposema: Sitaweza kulikomboa, liwe langu, nisiliharibu fungu langu. Likomboe wewe, liwe lako lililonipasa mimi, nilikomboe. Kwani siwezi kulikomboa.
7Tena kale kwa Waisiraeli ilikuwa desturi, walipokomboa, au waliponunua shamba, wakitaka kulishupaza hilo jambo la namna hii, mtu avue kiatu chake kimoja, ampe mwenzake; huu ulikuwa ushuhuda kwao Waisiraeli.[#5 Mose 25:7-10.]
8Kwa hiyo, yule mwingiliaji alipomwambia Boazi: Linunue, liwe lako! akakivua kiatu chake.
9Ndipo, Boazi alipowaambia wale wazee nao watu wote: Ninyi m mashahidi leo hivi, ya kuwa nimeyapata mkononi mwa Naomi yote yaliyokuwa yake Elimeleki nayo yote yaliyokuwa ya Kilioni na ya Maloni.
10Naye Ruti wa Moabu, mkewe Maloni, nimempata, awe mke wangu, nilikalishe jina lake aliyekufa katika fungu lake, hilo jina lake aliyekufa lisiangamie kwa ndugu zake wala malangoni mahali pake, alipokuwa. Ninyi m mashahidi leo hivi.
11Ndipo, watu wote waliokuwako malangoni nao wazee wale waliposema: Tu mashahidi. Bwana na amfanye huyu mwanamke aliyeingia nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea walioijenga wote wawili nyumba ya Isiraeli! Pata nguvu mle Efurata, jina lako litajwe mle Beti-Lehemu!
12Nao mlango wako uwe kama mlango wa Peresi, Tamari aliyemzalia Yuda, nao utoke katika wazao, Bwana atakaokupa kwa kijana huyu![#1 Mose 38:29.]
13Ndivyo, Boazi alivyomchukua Ruti, akawa mkewe, akaingia nyumbani mwake, Bwana akampa kuwa mwenye mimba, akazaa mtoto wa kiume.[#Sh. 127:3.]
14Ndipo, wanawake walipomwambia Naomi: Bwana na atukuzwe, kwa kuwa hakukuacha leo, ukose mwingiliaji. Jina lake huyu na litangazwe kwao Waisiraeli,
15naye na akutulize roho yako kwa kukutunza vema katika uzee wako. Kwani mkweo anayekupenda, akufanyiziaye mema kuliko wana saba wa kiume, ndiye aliyemzaa.
16Kisha Naomi akamchukua yule mtoto, akamweka kifuani pake, akawa mlezi wake.
17Nao wanawake wenzake, waliokaa nao, wakamwita jina kwamba: Naomi amezaliwa mwana wa kiume, wakamwita jina lake Obedi (Mtumishi), naye ni babake Isai aliye babake Dawidi.[#Mat. 1:5-6; Luk. 3:32.]
(18-22: Mat. 1:3-6.)18Hawa ndio walio wa uzao wa Peresi: Peresi alimzaa Hesironi,[#1 Mose 46:12; 1 Mambo 2:5.]
19Hesironi akamzaa Ramu, Ramu akamzaa Aminadabu,
20Aminadabu akamzaa Nasoni, Nasoni akamzaa Salmoni,[#1 Mambo 2:9-15; 4 Mose 1:7.]
21Salmoni akamzaa Boazi, Boazi akamzaa Obedi.
22Obedi akamzaa Isai, Isai akamzaa Dawidi.[#1 Sam. 16:1,11-13.]