The chat will start when you send the first message.
1Mwombeni Bwana mvua siku za vuli!
Bwana ndiye afanye mawingu yenye umeme;
naye ndiye anayewapa matone ya mvua,
majani yote ya shambani yaipate.
2Kwani vinyago husema yasiyo na maana,
nao waaguaji huona yaliyo uwongo,
husema ndoto zisizo za kweli,
wakituliza mioyo, ni bure;
kwa hiyo watu hujiendea kama kondoo,
huteseka, kwani hakuna awachungaye.
3Wachungaji ndio, makali yangu yanaowawakia moto,
nao viongozi ndio, nitakaowapatiliza;
kwani Bwana Mwenye vikosi amelikagua kundi lake,
ndio mlango wa Yuda,
nao ndio atakaowageuza,
wawe kama farasi mwenye utukufu wake katika mapigano.
4Kwao ndiko, kutakakotoka jiwe la pembeni,
hata uwambo wa hema,
hata upindi wa kupigania,
kweli kwao ndiko, watakakotokea wote pia waongozao vikosi.
5Nao watakuwa kama mafundi wa vita,
wawakanyagao adui matopeni barabarani kwenye mapigano;
watakapopigana, Bwana atakuwa nao,
wawatweze waliopanda farasi.
6Nitawatia nguvu walio mlango wa Yuda,
nao walio mlango wa Yosefu nitawaokoa,
nitawarudisha kwao, kwani nitawahurumia,
nao watakuwa kama watu, nisiowatupa
kwani mimi Bwana ni Mungu wao, nami nitawaitikia.
7Nao Waefuraimu watakuwa kama mafundi wa vita,
nayo mioyo yao itafurahiwa kama yao waliokunywa mvinyo;
wana wao watakapoyaona, watafurahi,
nayo mioyo yao itashangilia kwa kuwa na Bwana.
8Nitawakusanya na kuwapigia miluzi, kwani nitawakomboa;
nao watakuwa wengi, kama walivyokuwa wengi kale.
9Nimewatawanya katika makabila mengine,
lakini huko mbali nako watanikumbuka;
kwa hiyo watapona pamoja na wana wao, wapate kurudi kwao.
10Nami nitawarudisha kwao na kuwatoa katika nchi ya Misri,
nitawakusanya na kuwatoa katika nchi ya Asuri,
niwapeleke katika nchi ya Gileadi na ya Libanoni,
lakini huko nako hawataenea wote.
11Watakapopita baharini penye masongano, atayapiga mawimbi pale baharini;
ndipo, mafuriko ya maji ya jito la Nili yatakapokupwa yote,
nayo majivuno ya Asuri yatanyenyekezwa,
nayo bakora ya kifalme ya Misri haitakuwa na budi kutoweka.
12Nami nitawatia nguvu za kuwa na Bwana,
wafanye mwenendo wao katika Jina lake;
ndivyo, asemavyo Bwana.