The chat will start when you send the first message.
1Siku hiyo ndipo, walio wa mlango wa Dawidi nao wenyeji wa Yerusalemu watakapofunuliwa kisima kwa ajili ya makosa na kwa ajili ya machafu.[#Yes. 12:3; 55:1.]
2Ndivyo, asemavyo Bwana: Siku hiyo ndipo, nitakapoyang'oa majina ya vinyago vyote katika nchi hii, visikumbukwe tena; hata wafumbuaji na roho zenye uchafu nitawaondoa, watoke katika nchi hii.[#Mika 5:12.]
3Itakuwa, kama mtu atataka kufumbua maneno tena, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia: Hutapata kuishi, kwani unasema uwongo na kulitaja Jina la Bwana, kisha baba yake na mama yake waliomzaa watamchoma kwa ajili ya ufumbuaji wake.[#5 Mose 13:5.]
4Siku hiyo ndipo, wafumbuaji watakapopatwa na soni, kila mmoja kwa ajili ya maono yake, atakapofumbua maneno, tena hatakuwako atakayevaa joho la manyoya ya nyama, apate kusema yaliyo uwongo.[#2 Fal. 1:8.]
5Ila atasema: Mimi si mfumbuaji, mimi ni mtu alimaye shamba, kwani tangu ujana wangu mtu alininunua, niwe mtumwa wake.
6Mtu atakapomwuliza: Haya makovu kifuani katikati ya mikono yako ni ya nini? atasema: Ni ya mapigo, niliyoyapata nyumbani mwao, niliowapenda.
7Wewe upanga, amka, umpige mchungaji wangu na mwenzangu wa bia! Ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi. Mpige mchungaji, kondoo watawanyike! Nami nitaugeuza mkono wangu, uwaelekeze wadogo.[#Mat. 26:31.]
8Ndivyo, asemavyo Bwana: Hapo ndipo, mafungu mawili yatakapoangamizwa katika nchi hii yote nzima, yafe, lakini fungu la tatu litasazwa huko.[#Yes. 6:13.]
9Nalo hilo fungu la tatu nitalitia motoni, niwang'aze kwa kuwayeyusha, kama watu wanavyong'aza fedha kwa kuiyeyusha, tena nitawajaribu kabisa, kama watu wanavyojaribu dhahabu. Kisha hapo, watakapolililia Jina langu, mimi nitawaitikia na kuwaambia: Hawa ndio walio ukoo wangu; ndipo, watakapoitikia wao: Nawe Bwana ndiwe Mungu wetu.[#Hos. 2:23; Mal. 3:2-3.]