Zakaria 9

Zakaria 9

Wamizimu watanyenyekezwa.

1Hili ndilo tamko zito la Bwana.

linaionya nchi ya Hadiraki na mji wa Damasko, lipate kutua humo, kwani Bwana ndiye, watu wanayemwelekezea macho

pamoja na koo zote za Isiraeli.

2Linaionya nchi ya Hamati inayopakana nao, hata Tiro na Sidoni,

kwani ni yenye werevu mwingi ulio wa kweli:

3Watiro walijijengea boma, wakalimbika fedha, kama ni mavumbi,

na dhahabu tupu kama ni taka za barabarani.

4Lakini mtaona, Bwana akiuteka,

azibwage mali zake pamoja na vikosi vyake baharini,

lakini wenyewe utateketezwa kwa moto.

5Askaloni utakapoyaona, utashikwa na woga;

nao Gaza utatetemeka sana, Ekroni nao,

kwa kuwa mji huo, walioungojea, utakuwa umewatia soni;

namo Gaza mfalme atatoweka namo Askaloni hawatakaa watu tena.

6Asdodi watakaa wana wa ugoni,

lakini nitayakomesha majivuno ya Wafilisti.

7Tena nitaziondoa nyama zao zenye damu vinywani mwao,

navyo vyakula vyao vitapishavyo nitaviondoa katika meno yao;

ndipo, nao walio masao yao watakapomjua Mungu wetu,

wawe kama mkuu kwao Wayuda, nao Waekroni wawe kama Wayebusi.

8*Kisha nitapiga kambi, iwe kilindo cha Nyumba yangu,

pasipite mtu kwenda na kurudi,

wala pasipite kwao tena mtesaji,

kwani tangu hapo nitawaangalia kwa macho yangu,

Kiagio cha Masiya

9Piga vigelegele sana, binti Sioni!

Shangilia, binti Yerusalemu!

Tazama, mfalme wako anakujia!

Ni mwongofu na mwokozi, tena ni mnyenyekevu,

amepanda punda aliye mwana bado

wa kuwa na mama yake.

10Ndipo, nitakapoyatowesha magari kule Efuraimu,

nao farasi mle Yerusalemu,

nazo pindi za vita zitatoweshwa,

nao wamizimu atawafundisha kutengemana;

ufalme wake utaanzia baharini, uifikie bahari ya pili,

tena uanzie penye jito kubwa, uyafikie mapeo ya nchi.

11Wafungwa wako wewe nitawakomboa kwa ajili ya damu ya agano lako,

niwatoe shimoni msimo na maji.

12Rudini ngomeni, ninyi wafungwa mliokishika kingojeo chenu!

Leo hivi nawaambia: Nitakurudishia mara mbili yaliyokuwa yako.*

13Kwani Wayuda ninawatumia kuwa upindi wangu,

nao Waefuraimu kuwa mishale;

kisha nitawaamsha wanao, Sioni, wawaendee wana wako, Ugriki;

ndipo, nitakapokugeuza kuwa kama upanga wa fundi wa vita

14Naye Bwana ataoneka kwao, mshale wake utokee kama umeme;

kisha Bwana Mungu atapiga baragumu

akija katika pepo kali za nchi ya kusini.

15Bwana Mwenye vikosi atawakingia kwa ngao yake,

waje kuwala wakiyakanyaga mawe ya makombeo,

watakunywa damu zao wakipiga makelele kama wanaokunywa mvinyo;

hivyo watajaa kama mabakuli

yachukuayo damu za ng'ombe za tambiko,

hivyo wenyewe watakuwa kama pembe za meza ya kutambikia.

16Ndivyo, Bwana Mungu wao atakavyowaokoa siku hiyo,

kwa kuwa ndio kundi lao walio ukoo wake,

tena ndio vito vya taji vinavyometameta katika nchi yake.

17Tazameni, wema wao na uzuri wao ulivyokuwa mwingi!

Ngano hukuza vijana wa kiume nazo pombe mbichi vijana wa kike.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania