The chat will start when you send the first message.
1Ndipo Bildadi huyo Mshuhi akajibu, na kusema,
2Wewe utanena maneno haya hadi lini?
Maneno ya kinywa chako yatakuwa kama upepo mkuu hadi lini?
3Je! Mungu hupotosha hukumu?[#Mwa 18:25; Kum 32:4; Ayu 34:12; Dan 9:14]
Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki?
4Kwamba watoto wako wamemfanyia dhambi,
Naye amewatia mkononi mwa kosa lao;
5Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii,
Na kumsihi huyo Mwenyezi;
6Ikiwa wewe u safi na mwelekevu;
Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako,
Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa.
7Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo,
Lakini mwisho wako ungeongezeka sana.
8Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani,[#Kum 4:32]
Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta;
9(Kwani sisi tu wa jana tu, wala hatujui neno,[#Mwa 47:9; Zab 39:5]
Kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli tu;)
10Je! Hawatakufunza wao, na kukueleza,
Na kutamka maneno yatokayo mioyoni mwao?
11Je! Hayo mafunjo yamea pasipo matope
Na makangaga kumea pasipo maji?
12Yakiwa yangali mabichi bado, wala hayakukatwa,[#Zab 129:6; Yer 17:6; Yak 1:10,11; 1 Pet 1:24]
Hunyauka mbele ya majani mengine.
13Ndivyo ulivyo mwisho wa hao wamsahauo Mungu;[#Ayu 11:20; 18:14; Zab 112:10; Mit 10:28; Isa 33:14; Mt 24:51; Lk 12:1,2]
Na matumaini yake huyo mbaya huangamia;
14Uthabiti wake utavunjika,
Na matumaini yake huwa ni utando wa buibui.
15Ataitegemea nyumba yake, isisimame;[#Ayu 27:18]
Atashikamana nayo, isidumu.
16Yeye huwa mti mbichi mbele ya jua,
Nayo machipukizi yake huenea katika bustani yake.
17Mizizi yake huzongazonga chuguu,
Huangalia mahali penye mawe.
18Lakini, aking'olewa mahali pake,[#Ayu 7:10; Zab 37:36]
Ndipo patamkana, na kusema, Mimi sikukuona.
19Tazama, furaha ya njia yake ni hii,[#Zab 113:7]
Na wengine watachipuka kutoka katika nchi.
20Tazama, Mungu hatamtupa mtu mkamilifu,[#Zab 37:24; 1 The 5:23,24]
Wala hatawathibitisha watendao uovu.
21Bado atakijaza kinywa chako kicheko,
Na midomo yako ataijaza shangwe.
22Hao wakuchukiao watavikwa aibu;
Nayo hema yake mwovu haitakuwako tena.