The chat will start when you send the first message.
1Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,
Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
2Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi,
Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.
3Maji yake yajapovuma na kuumuka,
Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.
4Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu,[#Isa 8:7; Ufu 22:1; 2 Nya 6:6; Zab 48:1; Isa 60:14; Ebr 12:22]
Patakatifu pa maskani zake Aliye Juu.
5Mungu yu katikati ya mji hautatetemeshwa;[#Kum 23:14; Isa 12:6; Eze 43:7]
Mungu atausaidia asubuhi na mapema.
6Mataifa yanaghadhibika na falme kutetemeka;
Anatoa sauti yake, nchi inayeyuka.
7BWANA wa majeshi yu pamoja nasi,
Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
8Njoni muyatazame matendo ya BWANA,
Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.
9Avikomesha vita hata mwisho wa dunia;
Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari.
10Tulieni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu,[#Kut 14:13; Isa 2:11]
Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.
11BWANA wa majeshi yu pamoja nasi,
Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu.