The chat will start when you send the first message.
1Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari?[#1 Sam 22:9-10; 21:7]
Wema wa Mungu upo sikuzote.
2Ulimi wako watunga madhara,[#Zab 50:19; Mit 12:18; Zab 59:7]
Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila.
3Umependa mabaya kuliko mema,[#Yer 9:4]
Na uongo kuliko kusema kweli.
4Umependa maneno yote ya kupoteza watu,
Ewe ulimi wenye hila.
5Lakini Mungu atakuharibu hata milele;[#Mit 2:22]
Atakuondolea mbali;
Atakunyakua hemani mwako;
Atakung'oa katika nchi ya walio hai.
6Nao wenye haki wataona;[#Ayu 22:19; Zab 58:10]
Wataingiwa na hofu na kumcheka;
7Kumbe! Huyu ndiye mtu yule,[#Ayu 31:24,25; Zab 49:6]
Asiyemfanya Mungu kuwa kimbilio lake.
Aliutumainia wingi wa mali zake,
Na kufanya mali kimbilio lake.
8Bali mimi ni kama mzeituni[#Zab 92:13]
Umeao katika nyumba ya Mungu.
Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.
9Nitakushukuru milele kwa maana umetenda;[#Zab 54:6]
Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema;
Mbele ya wacha Mungu wako.