Zab 4

Zab 4

Ombi la Kuokolewa kutoka kwa Adui

1Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo;

Umenifanyizia nafasi wakati wa shida;

Unifadhili na kuisikia sala yangu.

2Enyi wanadamu, hata lini utukufu wangu utafedheheka?

Je! Mtapenda ubatili na kutafuta uongo?

3Bali jueni ya kuwa BWANA amejiteulia mtauwa;[#Kut 33:16; 2 Pet 2:9]

BWANA atasikia nimwitapo.

4Mwe na hofu wala msitende dhambi,[#Efe 4:26; Mit 3:7]

Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.

5Toeni dhabihu za haki,[#Kum 33:19; Zab 37:3]

Na kumtumaini BWANA.

6Wengi husema, Nani atakayetuonyesha mema?[#Zab 80:3]

BWANA, utuinulie nuru ya uso wako.

7Umenitia furaha moyoni mwangu,

Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai.

8Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara,[#Law 26:5; Kum 12:10; Yn 14:27; Flp 4:7]

Maana Wewe, BWANA, peke yako,

Ndiwe unijaliaye kukaa salama.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania