The chat will start when you send the first message.
1Enyi watu wote, pigeni makofi,
Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe.
2Kwa kuwa BWANA Aliye juu, mwenye kuogofya,[#Kum 7:21; Neh 1:5; Mal 1:14]
Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote.
3Atawatiisha watu wa nchi chini yetu,[#Zab 18:47]
Na mataifa chini ya miguu yetu.
4Atatuchagulia urithi wetu,[#1 Pet 1:4]
Fahari ya Yakobo ambaye alimpenda.
5Mungu amepaa kwa kelele za shangwe,[#Zab 24:7-10; Mdo 1:9; Efe 4:8-10; 1 Tim 3:16]
BWANA kwa sauti ya baragumu.
6Mwimbieni Mungu, naam, imbeni;
Mwimbieni mfalme wetu, naam, imbeni.
7Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote,[#Zek 14:9; 1 Kor 14:15]
Imbeni kwa akili.
8Mungu awamiliki mataifa,
Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu.
9Wakuu wa watu wamekusanyika,
Wawe watu wa Mungu wa Ibrahimu.
Maana ngao za dunia zina Mungu,
Ametukuka sana.