The chat will start when you send the first message.
1NAWAARIFU, ndugu, injili niliyowakhubirieni; ndiyo mliyoipokea, katika hiyo mnasimama,
2na kwa hiyo mnaokolewa, ikiwa mnayashika sana maneno niliyowakhuhirieni; isipokuwa mliamini burre.
3Kwa maana naliwapasha khabari ya mambo niliyoyapokea, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko;
4na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko;
5na ya kuwa alionekana na Kefa; tena na wathenashara;
6baadae alionekana na ndugu zaidi ya khamsi mia pamoja; katika hao walio wengi wanaishi hatta sasa, wengine wamelala;
7baadae alionekana na Yakobo; tena na mitume wote;
8na mwisho wa watu wote, alionekana na mimi, kama nae aliyezaliwa si kwa wakati wake.
9Maana mimi mdogo katika mitume, nisiyestahili kutajwa mtume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu.
10Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si burre, bali nalizidi sana kushika kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali neema ya Mungu pamoja nami.
11Bassi, kama ni mimi, kama ni wale, ndivyo tukhubirivyo, na ndivyo mlivyoamini.
12Bassi, ikiwa Kristo amekhubiriwa kwenu ya kwamba amefufuka, mbona wengine wenu wasema kwamba hakuna kiyama ya wafu?
13Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo nae hakufufuliwa:
14tena kama Kristo hakufufuliwa, bassi, kukhubiri kwetu ni burre na imani yenu ni burre.
15Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uwongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambae hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.
16Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo nae hakufufuliwa.
17Na kama Kristo hakufufuliwa, imani yenu ni burre; mngali katika dhambi zenu.
18Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea.
19Kama katika maisha haya tu tumemtumainia Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote.
20Lakini sasa Kristo amefufuka, limbuko lao waliolala.
21Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu.
22Kwa kuwa katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.
23Lakini killa mmoja mahali pake; limbuko Kristo; baadae walio wake Kristo, atakapokuja.
24Ndipo palipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.
25Maana sharti amiliki yeye, hatta awaweke maadui wote chini ya miguu yake.
26Adui wa mwisho atakaebatilishwa ni mauti.
27Kwa kuwa alitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini akisema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hamo.
28Bassi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe nae atatiishwa chini yake aliyemtiishia vitu vyote, illi Mungu awe yote katika yote.
29Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu watafanyaje, bassi, kama wafu hawafufuki?
30Kwa nini wakabatizwa kwa ajili yao? Na sisi, kwa nini tumo khatarini killa saa?
31Naam, kwa huku kujisifu kwangu niliko nako juu yenu katika Kristo Yesu Bwana wetu, ninakufa killa siku.
32Ikiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nalipigana na nyama wakali kule Efeso, nina faida gani wasipofufuka wafu? Tule, tukanywe, maana kesho tutakufa.
33Msidanganyike: mazumgumzo mabaya huharibu tabia njema.
34Erevukeui kama ipasavyo, wala insiteude dhambi; kwa maana wengine hawamfahamu Mungu. Ninasema haya niwafedheheshe.
35Labda mtu atasema, Wafufukaje wafu? Na kwa mwili gani waja?
36Mpumbavu! uipandayo wewe haihuiki, isipokufa;
37nayo uipandayo, huupandi mwili ule utakaokuwa, illa punje tupu, ikiwa ya nganu au nyingineyo;
38lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo, na killa mbegu mwili wake.
39Nyama yote si nyama moja; bali nyingine ya wana Adamu, nyingine ya ngʼombe, nyingine ya ndege, nyingine ya samaki.
40Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fakhari yake ya mbingu ni mbali, na fakhari yake ya duniani mbali.
41Fakhari ya jua mbali, na fakhari ya mwezi mbali, na fakhari ya nyota mbali; maana iko tofauti ya fakhari kati ya nyota na nyota.
42Kadhalika na kiyama ya wafu. Hupandwa katika nharibifu; hufufuka pasipo nharibifu;
43hupandwa katika aibu; hufufuka katika fakhari; hupandwa katika udhaifu; hufufuka katika nguvu;
44hupandwa mwili wa asili; hufufuka mwili wa roho. Ikiwa upo mwili wa asili, na wa roho upo.
45Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza Adamu alikuwa nafsi hayi; Adamu wa mwisho roho yenye kuhuisha.
46Lakini hautangulii wa roho, bali wa asili; baadae huja wa roho.
47Mtu wa kwanza atoka katika inchi, wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni.
48Alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni.
49Na kama tulivyoichukua sura yake wa udongo, kadhalika tulaichukua sura yake wa mbinguni.
50Nisemayo ni haya, ndugu, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharihika.
51Angalieni, nawaambieni siri; hatutalala wote, lakini wote tutabadilika,
52kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa panda la mwisho; maana panda litalia, na wafu watafufuka, wasiwe na uharibifu, na sisi tutahadilika.
53Maana sharti huu wenye uharibifu uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.
54Bassi, uharibifu huu utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.
55U wapi, mauti, uchungu wako? Ku wapi, kaburi, kushinda kwako?
56Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni sharia.
57Lakini tumshukuru Mungu atupae kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
58Bassi, ndugu wapendwa, mwe imara, msiotikisika, mkizidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa taabu yenu siyo burre katika Bwana.