1 Petro 4

1 Petro 4

1BASSI kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake kwa ajili yenu, ninyi nanyi jivikeni nia ile ile kama silaha; kwa maana yeye allyeteswa katika mwili, ameachana na dhambi;

2kuanzia sasa tusiendelee kuishi katika tamaa za wana Adamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wetu wa kukaa hapa duniani uliobakia.

3Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda wayapendayo mataifa, kuenenda katika uasharati, ua tamaa, na ulevi, ua karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali:

4mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao hatta ufisadi usio kiasi, wakiwatukaneni;

5watakaotoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hayi na waliokufa.

6Maana kwa ajili hiyo na wao waliokufa walikhubiriwa Injili, illi waluikumiwe katika mwili wahukumiwavyo wana Adamu; bali wawe hayi katika roho kwa kumtii Mungu.

7Mwisho wa mamho yote umekaribia; bassi, mwe na akili, mkakeshe katika sala:

8zaidi ya yote mwe na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husetiri wingi wa dhambi;

9mwe wakaribishaji ninyi kwa ninyi, pasipo kunnngʼunika;

10killa mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kukhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.

11Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akikhudumu, na akhudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; illi Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo; utukufu na uweza u kwake hatta milele na milele. Amin.

12Wapenzi, msione kuwa ni ajahu ule msiba unaowapata kama moto illi mjaribiwe, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho;

13lakini kama mnavyoyashiriki mateso va Kristo furahini; illi na katika ufimuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe.

14Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni kheri yenu, kwa kuwa Roho ya utukufu na ya Mungu unawakalia; kwa hawo anatukanwa, bali kwenu ninyi anatukuzwa.

15Maana mtu wa kwenu asiteswe kama muuaji, au mwizi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishae na mambo ya watu wengine.

16Illakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hili.

17Kwa maana wakati umefika hukumu ianzie nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu, nini mwisho wao wasioitu Injili ya Mungu?

18Na mwenye haki akiokoka kwa shidda, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi?

19Bassi wao wateswao apendavyo Mungu na wamwekee roho zao kama amana, katika kutenda mema, kama kwa Muumba mwaminifu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania