The chat will start when you send the first message.
1PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kama alivyopenda Mungu, kwa ahadi ya uzima ulio katika Yesu Kristo:
2kwa Timotheo mwanangu mpendwa; Neema, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.
3Namshukuru Mungu, nimwabuduye tangu zamani za wazee wangu kwa dhamiri safi, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu, mchana na usiku, ninatamani sana kukuona,
4nikikumbuka machozi yako, illi nijae furaha;
5nikikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, iliyokaa kwanza katika bibi yako Loi, na katika mama yako Euniki; aa ninasadiki ya kwamba na wewe nawe unayo.
6Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu.
7Maana Mungu hakutupa roho ya khofu, bali ya nguvu na ya upendo ua ya moyo wa kiasi.
8Bassi usiutahayarikie ushuhuda wa Bwana wetu, wala mimi mtumwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja na Injili kwa kadiri ya nguvu ya Mungu;
9aliyetuokoa akatuita kwa wito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu, bali kwa kadiri ya makusudi yake mwenyewe na neema yake, tuliyopewa sisi katika Kristo Yesu, kabla ya nyakati za zamani;
10na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Yesu Kristo, aliyebatili mauti na kuufunua uzima ua kutoa kuharibika, kwa ile Injili,
11aliyonifauya mkhubiri na mtume na mwalimu wa mataifa.
12Kwa sababu hiyo nimepata mateso haya, wala sitahayariki: maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki kwamba aweza kukilinda kile nilichakiweka amana kwake hatta siku ile.
13Shika sura ya maneno yenye uzima uliyoyasikia kwangu, katika imani na upendo uiio katika Kristo Yesu.
14Ilinde ile amana nzuri kwa Rolio Mtakatifu akaae ndani yetu.
15Wajua hili, ya kuwa wote walio katika Asia wameniacha, katika hao ni Figello na Hermogene.
16Bwana awape rehema walio wa uyumba ya Onesiforo; maana marra nyingi aliniburudisha, wala hakuutahayarikia mnyororo wangu;
17bali, alipokuwa katika Rumi, alinitafuta kwa bidii, akanipata.
18Bwana na ampe kuona rehema kwa Bwana siku ile. Na jinsi alivyonikhudumia katika Efeso, wewe wajua sana.