The chat will start when you send the first message.
1BASSI wewe, mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu.
2Na yale uliyoyasikia kwangu kwa mashahidi wengi, uwakabidbi hayo watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.
3Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Yesu Kristo.
4Hakuna mfanya vita ajitiae katika shughuli za dunia; illi ampendeze yeye aliyemwandika awe askari.
5Hatta mtu akishindana hapewi taji asiposhindana kwa halali.
6Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa kwanza wa kuyashiriki matunda.
7Yafahamu sana hayo nisemayo, maana Bwana atakupa akili katika mambo yote.
8Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuka katika wafu, wa uzao wa Daud, kama inenavyo injili yangu.
9Katika huyu nimeteswa kiasi cha kufungwa, kama mtenda mabaya; illakini neno la Mungu halifungwi.
10Kwa ajili ya hilo nastahimili yote, kwa ajili ya wateule, wao nao waupate wokofu ulio katika Kristo Yesu pamoja ua utukufu wa milele.
11Neno hili ni neno la kuaminiwa. Maana kama tukifa pamoja nae, tutaishi pamoja nae pia;
12kama tukistahimili, tutamiliki pamoja nae pia; kama tukimkana yeye, yeye nae atatukana sisi:
13ikiwa hatuamini, yeye hudumu kuwa mwaminifu, hawezi kujikana nafsi yake.
14Uwakumbushe bayo, ukiwaonya katika Bwana, wasiwe na mashindano ya maneno, yasiyo na faida, bali huwaharibu wasikiao.
15Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiyetahayarishwa, ukitumia kwa halali neno la Mungu.
16Jiepushe na maneno yasiyo na maana, yasiyo ya dini; maana wataendelea zaidi katika maovu;
17na neno lao litakuwa likitafuna kama donda ndugu. Katika hao ni Humenayo na Fileto,
18walioikosa kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, nao waipindua imani ya watu wengine.
19Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake; tena, killa alilajae jina la Bwana na aache uovu.
20Bassi katika nyumba havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina heshima.
21Bassi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hawa atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa killa kazi iliyo njema.
22Lakini zikimbie tamaa za ujana; nkafuate haki, na imani, na uaminifu, na upendo, na amani, pamoja na hao wamwitiao Bwana kwa moyo safi.
23Walakini yakatae maswali ya upumbavu, yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi:
24Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi, bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezae kufundisha, mvumilivu,
25akiwaonya kwai npole washindanao nae, illi, kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na ujuzi wa kweli,
26wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Shetani, wamepatikana wahayi nae, hatta kuyafanya apendayo Mungu.