Matendo 25

Matendo 25

1HATTA Festo alipokwisha kuingia katika wilaya yake, baada ya siku tatu akapanda kwenda Yerusalemi kutoka Kaisaria.

2Kuhani mkuu na Wayahudi wakampasha khabari za Paolo, wakamsihi,

3na kumwomba awafadhili, na kutoa amri aletwe Yerusalemi, wapate kumwotea na kumwua njiani.

4Festo akajibu ya kama Paolo atalindwa Kaisaria; nae mwenyewe yu tayari kwenda huko karibu.

5Akasema, Wale walio na mamlaka na watelemke pamoja nami wakamshitaki, ikiwa liko neno baya katika mtu huyu.

6Alipokwisha kukawia kwao siku kumi na zaidi, akatelemkia Kaisaria: hatta siku ya pili akaketi katika kiti cha hukumu akaamuru Paolo aletwe.

7Walipokuja Wayahudi walioshuka kutoka Yerusalemi wakasimama karibu yake wakaleta mashitaka mengi na mazito juu yake, wasiyoweza kuyathuhutisha.

8Paolo akajitetea hivi, ya kama, Mimi sikukosa neno juu ya sharia ya Wayahudi, wiila juu ya hekalu wala juu ya Kaisari.

9Lakini Festo akitaka kujipendekeza kwa Wayahudi akamjibu Paolo, akisema, Wataka kwenda Yerusalemi, ukahukumiwe huko mbele yangu?

10Paolo akasema, Mimi ninasimama hapa mbele ya kiti cha hukumu cha Kaisari, panipasapo kuhukumiwa: sikuwakosa Wayahudi neno, kama wewe ujuavyo sana.

11Ikiwa nimekosa au nimetenda neno la kustahili kufa, sikatai kufa; hali, kama si kweli neno hili wanalonishitaki, hapana awezae kunitia mikononi mwao. Nataka rufaani kwa Kaisari.

12Bassi Festo alipokwisha kusema na watu wa baraza, akajibu, Umetaka rufaani kwa Kaisari! bassi, utakwenda kwa Kaisari.

13Siku kadha wa kadha zilipokwisha kupita, Agrippa mfalme na Bereniki wakafika Kaisaria, wakimwamkia Festo.

14Na walipokuwa wakikaa huko siku nyingi, Festo akamweleza mfalme khabari za Paolo, akisema, Yupo hapa mtu aliyeachwa na Feliki kifungoni;

15nami nilipokuwa Yerusalemi makuhani wakuu na wazee wa Wayahudi wakaniarifu khabari zake, wakitaka ahukumiwe.

16Nikawajibu kwamba sio desturi ya Warumi kumtoa mtu aliye yote auawe, kabla mtu yule aliyeshitakiwa hajaonana na washitaki wake uso kwa uso, na kupewa nafasi ya kujitetea katika mashitaka yake.

17Bassi walipokutanika hapa sikukawia; bali siku ya pili nikaketi katika kiti cha hukumu nikaamuru mtu huyo aletwe.

18Na wale waliomshitaki waliposimama karibu nae, hawakumshitaki neno baya, kama nilivyodhani,

19hali walikuwa na maswali juu yake katika dini yao wenyewe, na katika khabari ya mtu mmoja Yesu, aliyekuwa amekwisha kufa, ambae Paolo alishika kusema kwamba yu hayi.

20Nami nikaona mashaka jinsi ya kutafuta hakika ya khabari hii, nikamwuliza kama anataka kwenda Yerusalemi ahukumiwe huko katika mambo haya.

21Lakini Paolo alipodai kuwekwa ahukumiwe na Augusto, nikaamuru alindwe hatta nitakapompeleka kwa Kaisari.

22Agrippa akamwambia Festo, Mimi nami nalikuwa nikitaka kumsikia mtu huyu. Akasema, Utamsikia kesho.

23Hatta assubuhi Agrippa akaja pamoja na Bereniki kwa fakhari nyingi, wakapaingia mahali pa kusikia maneno, pamoja na maakida na watu wakuu wa mji: Festo akatoa amri Paolo aletwe.

24Festo akasema, Mfalme Agrippa, na ninyi nyote mliopo hapa pamoja nasi, mnamwona mtu huyu, ambae jamii yote ya Wayahudi huku Yerusalemi na hapa pia wamenitaka niwasaidie, wakipiga kelele kwamba haimpasi kuzidi kuishi.

25Nami nilipoona kama hakutenda neno la kustahili kuuawa, na yeye mwenyewe alipotaka kuhukumiwa na Augusto, nalikusudia kumpeleka kwake.

26Nami sina neno la hakika la kumwandikia Bwana. Kwa hiyo nimemleta hapa mbele yenu, illi akiisha kuulizwa khabari zake, nipate neno la kuandika.

27Kwa maana naona ni neno lisilo maana kumpeleka mfungwa, bila kuonyesha mashitaka yale aliyoshitakiwa.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania