The chat will start when you send the first message.
1KRISTO alitufanya huru kwa uhuru; bassi, simameni, msinaswe tena kwa kifungo cha utumwa.
2Fahamuni, mimi Paolo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno.
3Tena namshuhudia killa mtu atahiriwae, kwamba ni wajibu wake kuitimiza sharia yote.
4Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kufanyiziwa wema kwa sharia; mmeanguka toka hali ya neema.
5Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la wema kwa njia ya imani.
6Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.
7Mlikuwa mkipiga mbio vizuri: ni nani aliyewazuia msiitii kweli?
8Kushawishi huku hakukutoka kwake yeye aliyewaita.
9Chachu kidogo huchachua donge nzima.
10Nina matumaini kwenu katika Bwana, kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine. Lakini yeye anaewafadhaisha atachukua hukumu yake awae yote.
11Na mimi, ndugu, ikiwa ninakhubiri khabari ya kutahiriwa, mbona ningali nikiudhiwa? Hapo kwazo la msaiaba limebatilika.
12Ningependa hawo wanaowatieni mashaka wangejikata nafsi zao.
13Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali khudumianeni kwa upendo.
14Maana sharia yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako.
15Lakini mkiumana na kulana angalieni msije mkaangamizana.
16Nasema, Enendeni kwa Roho, nanyi hamtatimiza tamaa za mwili.
17Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho hushindana na mwili; kwa maana liizi zimepingana, hatta hamwezi kufanya nmayotaka.
18Lakini nikiongozwa na Roho, hunpo chini ya sharia.
19Na matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasharati, uchafu, ufasiki,
20ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, nzushi,
21husuda, ulevi, ulafi, na yanayofanana na haya; juu ya haya nawaambieni mapema, kama nilivyokwisha kuwaambieni, watu watendao mambo ya jinsi hii hawatanrithi ufalme wa Mungu.
22Lakini matunda ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23upole, kiasi; juu ya mambo ya jinsi hii hapana sharia.
24Nao walio watu wa Kristo Yesu wameusulibisha niwili pamoja na mawazo mabaya na tamaa mbaya.
25Tukiisbi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.
26Tusijisifu burre, tukichokozana na kuhusudiana.