The chat will start when you send the first message.
1KWA hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi yaliyasikiwa tusije tukayakosa.
2Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na killa kosa na uasi ulipata ujira wa haki,
3sisi je! tutapataje kujiponya, tusipotunza wokofu mkiju namna hii? ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kiisha nkathubutika kwetu na wale waliosikia;
4Mungu nae akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa karama za Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.
5Maana hakuuweka chini ya malaika ulimwengu ule ujao tunaounena,
6illa mtu mmoja ameshuhudu hivi maliali fullani, Mwana Adamu ni nini hatta umkumbuke, ama mwana wa binadamu hatta umwangalie?
7Umemfanya mdogo punde kuliko malaika, umemvika taji ya utukufu na heshima, umemweka jua ya kazi za mikono yako;
8nmetia vitu vyote chini ya uyayo zake. Kwa maana katika kutia vitu vyote chini yake hakusaza kitu kisichotiwa. Illakini sasa hado hatujaona vitu vyote kutiwa chini yake,
9illa twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, illi kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya killa mtu.
10Kwa kuwa ilimpasa veye, ambae kwa ajili yake na kwa kazi yake vitu vyote vimekuwa, akileta wana wengi hatta utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokofu wao kwa mateso.
11Maana yeye atakasae nao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake;
12akinena, Nitalikhubiri jina lako kwa ndugu zangu; kati kati ya kanisa nitakuimba,
13na tena, Nitamtumaini: na tena, Tazama, mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu.
14Bassi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye nae vivyo hivyo alishiriki yayo bayo, illi kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani Shetani,
15akawaokoe wale ambao kwamba maisha zao zote kwa khofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa.
16Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, illa atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu.
17Kwa hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, illi afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.
18Na kwa kuwa aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.