Waebrania 3

Waebrania 3

1KWA hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki wito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu,

2Yesu, aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemfanya, kama Musa nae alivyokuwa katika nyumba yake yote.

3Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahili utukufu zaidi kuliko Musa, kamti vile yeye aitengenezae nyumba alivyo na heshima zaidi ya nyumba hiyo.

4Maana killa nyumba imetengenezwa na mtu; illa yeye aliyevitengeneza vitu vyote ni Mungu.

5Na Musa alikuwa mwaminifu katika nyumba yake yote kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa;

6bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba yake; ambae nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na kujisifu kwetu, kwa kutumaini mpaka mwisho.

7Kwa hiyo, kama anenavyo Robo Mtakatifu, Leo, kama mtasikia sauti yake,

8msifanye migumu mioyo yenu, kama wakati wa kunikasirisha, siku ya kujaribiwa katika jangwa,

9hapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima, wakaona matendo yangu miaka arubaini.

10Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki nikasema, Ni watu waliopotoka mioyo hawa; hawakujua njia zangu;

11kama nilivyoapa katika hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu.

12Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hayi.

13Lakini muonyane killa siku, maadam iitwapo leo; mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.

14Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu mpaka mwisho;

15hapo inenwapo, Leo, kama mtasikia sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu kama wakati wa kunikasirisha.

16Maana ni nani waliomkasirisha, waliposikia? Si wale wote waliotoka katika Misri wakiongozwa na Musa?

17Na ni nani aliochukizwa nao miaka arubaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa?

18Na ni nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika raha yake, illa wale wasioamini?

19Bassi twaona ya kuwa bawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania