The chat will start when you send the first message.
1BASSI, nauliza. Mungu aliwasukumia mbali watu wake? Hasha! maana mimi nami ni Mwisraeli, mmoja wa wazao wa Ibrahimu, mtu wa kabila ya Benjamin.
2Mungu hakuwasukumia mbali watu wake aliowajua tokea asili. Au hamjui yale yaliyonenwa na maandiko juu ya Eliya? jinsi anavyowashitaki Waisraeli mbele ya Mungu,
3Bwana, wamewaua nabii zakowamezibomoa madhbabu zako, nami mmesalia peke yangu, nao wanatafuta roho yangu.
4Lakini ile jawabu yamwanibiaje? Nimejisazia watu elfu saba wasiopiga goti mbele ya Baal.
5Bassi ni vivi hivi wakati huu wa sasa, yako maliaki waliochaguliwa kwa neema ya Mungu.
6Lakini ikiwa ni kwa neema yake, haiwi kwa matendo tena, au hapo neema isingekuwa neema; na ikiwa ni kwa matendo, haiwi neema tena, au hapo matendo yasingekuwa matendo.
7Imekuwaje bassi? Kitu kile ambacho Israeli alikuwa akikitafuta hakukipata, lakini wale waliochaguliwa walikipata, na wengine walitiwa ugumu.
8Kama ilivyoandikwa, Mungu aliwapa roho ya usingizi, macho hatta wasione, na masikio hatta wasisikie mpalla leo.
9Na Daud asema,
Meza yao iwe tanzi na mtego,
Na kitu cha kuwakwaza, na malipo kwao;
10Macho yao yatiwe giza wasione,
Ukawainamisbe mgongo wao siku zote.
11Bassi nasema, Je! wamejikwaa hatta wameanguka kabisa? Hasha! Lakini kwa kosa lao wokofu umewafikilia mataifa, illi wao watiwe wivu:
12bassi ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa ulimwengu, na upungufu wao umekuwa utajiri wa mataifa, je! si zaidi sana utimilifu wao?
13Lakini nasema na ninyi, watu wa mataifa. Kwa kadiri nilivyo mtume wa watu wa mataifa, naifukuza khuduma iliyo yangu.
14Huenda nikapata kuwatia wivu walio damu moja na mimi na kuwaokoa baadhi vao.
15Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhayi baada ya kufa?
16Tʼena malimbuko yakiwa matakatifu, vivyo hivyo na, donge lote; na shina likiwa takatifu, matawi nayo vivyo hivyo.
17Lakini iwapo matawi mengine yamekatiwa, na wewe mzeituni mwitu ulitiwa kati yao ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake,
18usijisifu juu ya matawi; au ikiwa wajisifu, si wewe ulichukuae shina bali shina likuchukualo wewe.
19Bassi utasema, Matawi yalikatiwa illi nitiwe mimi.
20Marra haba. Yalikatiwa kwa kutokuamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako. Usijivune bali uogope;
21kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili, wala hatakuachia wewe.
22Fahamu, bassi, wema na ukali wa Mungu; kwa wale walioanguka ukali, bali kwako wema, ukikaa katika wema huo; kama sivyo, wewe nawe utakatiliwa mbali.
23Na hao pia, wasipokaa katika kulokuamini kwao, watatiwa, kwa maana Mungu aweza kuwatia temi.
24Kwa maana ikiwa wewe ulikatwa ukatolewa katika mzeituni ulio mzeituni mwitu kwa asili yake, ukatiwa, kinyume cha asili, katika mzeituni ulio mwema; si zaidi sana wale walio wa asili watatiwa katika mzeituni wao wenyewe.
25Kwa maana sitaki ndugu msiijue siri hii, ms jione kuwa wenye akili, ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka ntimilifu wa mataifa uwasili;
26na hivi Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa,
Yeye aokoae atakuja kutoka Sayuni
Atamtenga Yakobo na maasi yake,
27Na hili ndilo agano langu nao,
Nitakapowaondolea dhambi zao.
28Bassi kwa khabari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu, bali kwa khabari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya haha zetu.
29Kwa sababu karama za Mungu na wito wake hazina majuto.
30Kwa maana kama ninyi zamani mlimwasi Mungu, lakini sasa mmepata rehema kwa kutokuamini kwao,
31vivyo hivyo na hao wameasi sasa, illi kwa kurehemiwa kwenu wao nao wapate rehema.
32Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi illi awarehemu wote.
33Ee ajabu ya utajiri na hekima na maarifa ya Mungu; hazina hatta kiasi! hukumu zake hazichunguziki, na njia zake hazitafutikani!
34Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake?
35Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, nae atalipwa?
36Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amin.