Warumi 2

Warumi 2

1KWA hiyo, ee mtu uhukumuye uwae yote, huna udhuru; kwa maana katika hayo uhukumuyo mwingine wajihukumu nafsi yako; kwa maana wewe uhukumuye unafanya yale yale.

2Na twajua ya kuwa hukumu ya Mungu ni ya kweli juu yao wafanyao hayo.

3Ee bin-Adamu, uwahukumuye wale wafanyao hayo na kutenda yayo hayo mwenyewe, je! wadhani ya kwamba utajiepusha na hukumu ya Mungu?

4Au waudharau wingi wa wema wake na uvumilivu wake na kusubiri kwake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvutia toba?

5bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu,

6atakaemlipa killa mtu kwa kadiri ya matendo yake;

7wale ambao kwa kustahimili katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoa kuharibika, nzima wa milele;

8na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, hasira na ghadhabu;

9mateso na shidda juu ya killa roho ya mwana Adamu atendae uovu, kwanza Myahudi na Myunani pia:

10bali utukufu na heshima na amani kwa killa mtu atendae mema, Myahudi kwanza na Myunani pia;

11kwa maana hapana upendeleo kwa Mungu.

12Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sharia watapotea pasipo sharia, na wote waliokosa, wakiwa na sharia, watahukumiwa kwa sharia.

13Kwa sababu sio waisikiao torati walio wenye haki mbele ya Mungu, bali ni wale waitendao torati watakaohesabiwa kuwa wenye haki.

14Kwa maana watu wa mataifu wasio na sharia wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, bao wasio na sharia wamekuwa sharia kwa nafsi zao wenyewe:

15hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na wakishitakiana killa mtu mwenzake kwa fikara zao na kuteteana;

16katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wana Adamu, sawa sawa na injili yangu, kwa Yesu Kristo.

17Lakini wewe, ukiwa unakwitwa Myahudi na kuitegemea torati, na kujisifu katika Mungu,

18na kuyajua mapenzi yake na kuyatambua manibo yaliyo bora, umeelimishwa katika torati,

19na kujua hakika ya kuwa wewe mwenyewe u kiongozi wa vipofu, mwanga wao walio gizani,

20mkufunzi wra wajiuga, mwalimu wa watoto wachanga, mwenye namna ya maarifa na ya kweli katika torati,

21hassi wewe umfundishae mwiugine, je! hujifimdishi nafsi yako? Wewe nkhubiriye kwamha mtu asiibe, waiba mwenyewe?

22Wewe usemae kwamba mtu asizini, wazini mwenyewe? Wewe uchukiae sanamu, wateka mahekidu?

23Wewe ujisifuye katika torati, kwa kuiasi torati wamvunjia Mungu heshima?

24Kwa maana jina la Mungu lanenwa unajisi katika mataifa kwa ajili yenu, kama ilivyoandikwa.

25Kwa maana kutahiriwa kwafaa kama ukiwa mtendaji wa sharia, lakini ukiwa mvunjaji wa sharia kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa.

26Bassi ikiwti yeye asiyetahiriwa huyashika maagizo ya torati, je! kutokutahiriwa kwake hakutahesahiwa kuwa kutahiriwa?

27Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikae torati, hatakuhukumu wewe, uliye na maandiko na kutahiriwa, ukaikhalifu torati?

28Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili;

29hali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; na sifa yake haitoki kwa wana Adamu hali kwa Mungu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania