Warumi 9

Warumi 9

1NASEMA kweli katika Yesu Kristo, sisemi uwongo, dhamiri yangu ikinishuhudia katika Roho Mtakatifu,

2ya kwamba nina huzuni nyingi na maumivu yasiyokoma moyoni mwangu.

3Kwa maana naliomba mimi mwenyewe niharamishwe na kutengwa na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, jamaa zangu kwa jinsi ya mwili;

4ambao ni Waisraeli, wenye kufanywa wana, wenye utukufu na maagano, wenye kupewa torati na ibada ya Mungu na ahadi zake; ambao mababu ni wao,

5na katika bao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili, aliye juu ya mambo yote, Mungu, anaehimidiwa milele. Amin.

6Si kana kwamba neno la Mungu limetanguka; maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli.

7Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali, Katika Isaak wazao wako watakwitwa;

8yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanabesabiwa kuwa wazao.

9Kwa maana neno la ahadi ni hili, Panapo wakati huu nitakuja, na Sara atakuwa na mwana.

10Wala si hivyo tu, lakini Rebeka nae, akiisha kuchukua mimba kwa mmoja, nae ni Isaak baba yetu—

11kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, illi lisimame kusudi la Mungu la kuchagua,

12si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitae aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo.

13Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia.

14Tuseme nini bassi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha!

15Maana alimwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiae.

16Bassi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakae, wala wa yule apigae mbio, bali wa yule arehemuye, yaani Mungu.

17Kwa maana maandiko yasema na Farao, ya kama, Nilikusimamisha, illi niouyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika inchi yote.

18Bassi, kama ni hivyo, atakae (kumrehemu) humrehemu, na atakae kumfanya mgumu humfanya mgumu.

19Bassi, utaniambia, Mbona angali akilaumu? Kwa maana nani aliyeshindana na kusudi lake?

20La! si hivyo, ee bin-Adamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Ya nini nkanifanza hivi?

21An mfinyangi je! bana nguvu juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kufanya chombo kimoja, kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?

22Bassi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake, na kujulisha uweza wake kwa uvumilivu mwingi alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu;

23tena ajulishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema alivyovitengeneza tangu zamani, vipate utukufu,

24ndio sisi tulioitwa nae, si watu wa Wayahudi tu, illa watu wa mataifa pia, utasemaje?

25Ni vile alivyosema katika Hosea,

Nitawaita wale kuwa watu wangu wasiokuwa watu wangu,

Na yeye mpenzi wangu asiyekuwa mpenzi wangu.

26Na itakuwa mahali pale walipoambiwa,

Ninyi si watu wangu,

Hapo watakwitwa wana wa Mungu aliye hayi.

27Isaya nae atoa santi yake juu ya Israeli, Hesabu ya wana wa Israeli, ijapokuwa kama mchanga wa bahari, ni mabaki yao tu watakaookolewa.

28Kwa maana Bwana atalitekeleza neno lake juu ya inchi, akilimaliza na kulikata.

29Na kama isaya alivyotangulia kunena,

Kama Bwana wa Sabaoth asingalituachia uzao,

Tungalikuwa kama Sodoma, tungalifananishwa na Gomora.

30Tuseme nini, bassi? Ya kwamba watu wa mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; yaani ile haki iliyo ya imani;

31bali Israeli wakiifuata sharia ya haki hawakuifikilia ile sharia.

32Kwa sababu gani? Kwa sababu hawakuitafuta kwa njia ya imani bali kana kwamba kwa njia ya matendo. Wakajikwaa juu ya jiwe lile likwaazalo,

33kama ilivyoandikwa,

Tazama, Naweka katika Sayuni jiwe likwaazalo, na mwamba uangushao:

Na killa amwaminiye hataaibishwa.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania