The chat will start when you send the first message.
1“Nimesumbuliwa vibaya tangu ujana wangu…”
Kila mtu katika Israeli na aseme:
2“Nimesumbuliwa vibaya tangu ujana wangu,[#129:2 Labda yahusu wakati Waisraeli walipokuwa bado Misri.]
lakini hawakufaulu kunishinda.
3Walinijeruhi vibaya mgongoni mwangu,
wakafanya kama mkulima anayelima shamba.
4Lakini Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu;
amezikata kamba za hao watu waovu.”
5Na waaibishwe na kurudishwa nyuma,
wote wale wanaouchukia mji wa Siyoni.
6Wawe kama nyasi juu ya paa la nyumba,[#129:6 Nyumba za huko Palestina wakati huo zilikuwa kwa wingi na mapaa yaliyo bapa. Mara nyingine majani yaliota juu yake, lakini mara nyingi joto la jua na ukosefu wa udongo wa kutosha uliyafanya kunyauka na hata kukauka kabisa.]
ambazo hunyauka kabla hazijakua,
7hakuna anayejishughulisha kuzikusanya,
wala kuzichukua kama matita.
8Hakuna apitaye karibu atakayewaambia:
“Mwenyezi-Mungu awabariki!
Twawabariki kwa jina la Mwenyezi-Mungu!”