Zaburi 67

Zaburi 67

Wimbo wa shukrani

1Utuonee huruma, ee Mungu, utubariki;

utuelekezee uso wako kwa wema;

2dunia yote ipate kutambua njia yako,[#67:2 Baraka wanazopata Waisraeli zitawafanya na watu wa mataifa wabarikiwe pia kama ahadi ile ya Mwa 12:1-3.]

mataifa yote yajue nguvu yako ya kuokoa.

3Watu wote wakutukuze, ee Mungu;

watu wote na wakusifu!

4Mataifa yote yafurahi na kuimba kwa furaha;

maana wawahukumu watu kwa haki,

na kuyaongoza mataifa duniani.

5Watu wote wakutukuze, ee Mungu;

watu wote na wakusifu!

6Nchi imetoa mazao yake;

Mungu, Mungu wetu, ametubariki.

7Mungu aendelee kutubariki.

Watu wote duniani na wamche.

Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993 The Bible Society of Kenya 1993
Published by: Bible Society of Tanzania