The chat will start when you send the first message.
1Basi Yefta Mgileadi alikuwa shujaa mwenye nguvu. Baba yake alikuwa Gileadi, naye mama yake alikuwa kahaba.
2Mke wa Gileadi pia akamzalia wana, nao walipokua, wakamfukuza Yefta, na kumwambia, “Wewe huwezi kupata urithi katika jamii yetu, kwa sababu wewe ni mwana wa mwanamke mwingine.”
3Basi Yefta akawakimbia ndugu zake akaenda kuishi katika nchi ya Tobu, mahali ambako watu waasi walijiunga naye na kumfuata.
4Baada ya muda Waamoni wakafanya vita na Israeli,
5viongozi wa Gileadi wakaenda kumchukua Yefta katika nchi ya Tobu.
6Wakamwambia Yefta, “Njoo, uwe jemadari wetu, ili tuweze kupigana na Waamoni.”
7Yefta akawaambia viongozi wa Gileadi, “Je, si mlinichukia na kunifukuza nitoke katika nyumba ya baba yangu? Kwa nini mwanijia sasa, wakati mko taabuni?”
8Viongozi wa Gileadi wakamwambia Yefta, “Lakini sasa tumegeuka kukuelekea wewe, ili uende pamoja nasi kupigana na Waamoni, nawe utakuwa kiongozi wetu juu ya watu wote wa Gileadi.”
9Yefta akawaambia viongozi wa Gileadi, “Ikiwa mtanirudisha kwetu kupigana na Waamoni, naye Bwana akanisaidia kuwashinda, je, ni kweli nitakuwa kiongozi wenu?”
10Viongozi wa Gileadi wakamjibu Yefta, “Bwana ndiye shahidi wetu. Kwa hakika tutafanya kama usemavyo.”
11Basi Yefta akaenda na viongozi wa Gileadi, nao watu wakamfanya kiongozi na jemadari wao. Naye akarudia maneno yake yote mbele za Bwana huko Mispa.
12Ndipo Yefta akatuma wajumbe kwa mfalme wa Waamoni akisema, “Una nini nasi, hata umekuja kushambulia nchi yetu?”
13Mfalme wa Waamoni akawajibu wajumbe wale wa Yefta, “Waisraeli walipopanda kutoka Misri, waliichukua nchi yangu kuanzia Mto Arnoni hadi Mto Yaboki, hadi kufikia Mto Yordani. Sasa irudishe kwa amani.”
14Yefta akarudisha wajumbe kwa mfalme wa Waamoni,
15kusema:
28Hata hivyo, mfalme wa Waamoni hakuyajali maneno ya ujumbe wa Yefta.
29Ndipo Roho wa Bwana akaja juu ya Yefta. Akapita katikati ya Gileadi na Manase, pia akapita katika Mispa ya Gileadi, na kutokea huko akasonga mbele kushambulia Waamoni.
30Naye Yefta akaweka nadhiri mbele za Bwana akisema, “Ikiwa utawatia Waamoni mikononi mwangu,
31chochote kile kitakachotoka katika mlango wa nyumba yangu cha kwanza ili kunilaki nirudipo kwa amani katika kuwashinda Waamoni, kitakuwa ni cha Bwana na nitakitoa kuwa sadaka ya kuteketezwa.”
32Ndipo Yefta akavuka kupigana na hao Waamoni, naye Bwana akawatia mkononi mwake.
33Akaharibu kabisa miji ishirini kuanzia Aroeri hadi karibu na Minithi, na kuendelea hadi Abel-Keramimu. Hivyo, Waisraeli wakawashinda Waamoni.
34Yefta aliporudi nyumbani mwake huko Mispa, tazama, binti yake akatoka ili kumlaki kwa matari na kucheza. Alikuwa mwanawe wa pekee, hakuwa na mwana wala binti mwingine.
35Alipomwona akararua mavazi yake akalia, “Ee! Binti yangu! Umenifanya niwe na huzuni na kunyongʼonyea sana, kwa kuwa nimeweka nadhiri kwa Bwana , ambayo siwezi kuivunja.”
36Akajibu, “Baba yangu, umetoa neno lako kwa Bwana . Nitendee mimi kama vile ulivyoahidi, kwa kuwa Bwana amekupa ushindi dhidi ya adui zako Waamoni.”
37Naye akamwambia baba yake, “Naomba nifanyiwe jambo hili. Nipewe miezi miwili ili kuzunguka vilimani nikaulilie ubikira wangu, mimi na wenzangu.”
38Baba yake akamwambia, “Unaweza kwenda.” Naye akamwacha aende kwa miezi miwili. Hivyo akaondoka pamoja na wenzake, naye akaulilia ubikira wake huko vilimani kwa sababu hangeolewa kamwe.
39Baada ya hiyo miezi miwili, alirejea kwa baba yake, naye baba yake akamtendea kama alivyokuwa ametoa nadhiri yake. Naye alikuwa bikira.
Nayo ikawa desturi katika Israeli,
40kwamba kila mwaka binti za Israeli huenda kwa siku nne ili kumkumbuka huyo binti Yefta Mgileadi.