Zaburi 108

Zaburi 108

Zaburi 108

Kuomba msaada dhidi ya adui

(Zaburi 57:7-11; 60:5-12)

1Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti;

nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote.

2Amka, kinubi na zeze!

Nitayaamsha mapambazuko.

3Nitakusifu wewe, Ee Mwenyezi Mungu, kati ya mataifa;

nitaimba habari zako, katika jamaa za watu.

4Kwa maana upendo wako ni mkuu, ni juu kuliko mbingu;

uaminifu wako unazifikia anga.

5Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,

utukufu wako na uenee duniani kote.

6Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume,

ili wale unaowapenda wapate kuokolewa.

7Mungu amenena kutoka patakatifu pake:

“Nitaigawa Shekemu kwa ushindi

na kulipima Bonde la Sukothi.

8Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu;

Efraimu ni chapeo yangu,

nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala.

9Moabu ni sinia langu la kunawia,

juu ya Edomu natupa kiatu changu;

nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.”

10Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome?

Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu?

11Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi,

na hutoki tena na majeshi yetu?

12Tuletee msaada dhidi ya adui,

kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu.

13Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi,

naye atawaponda adui zetu.

Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.