The chat will start when you send the first message.
1Ee Bwana , usinikemee katika hasira yako,
wala usiniadhibu katika ghadhabu yako.
2Unirehemu Bwana ,
kwa maana nimedhoofika;
Ee Bwana , uniponye,
kwa maana mifupa yangu
ina maumivu makali.
3Nafsi yangu ina uchungu mwingi.
Hadi lini, Ee Bwana , hadi lini?
4Geuka, Ee Bwana , unikomboe,
uniokoe kwa sababu ya fadhili zako.
5Hakuna mtu anayekukumbuka
akiwa amekufa.
Ni nani awezaye kukusifu
akiwa Kuzimu?
6Nimechakaa kwa kulia kwa huzuni;
usiku kucha natiririsha
kitanda changu kwa machozi;
nimelowesha kiti changu
kwa machozi yangu.
7Macho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika,
yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote.
8Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya,
kwa maana Bwana amesikia kulia kwangu.
9Bwana amesikia kilio changu kwa huruma,
Bwana amekubali sala yangu.
10Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika,
watarudi nyuma na waaibishwe kwa ghafula.