The chat will start when you send the first message.
1Ee BWANA, utanisahau hadi lini, hata milele?[#Kum 31:17; Ayu 13:24; Zab 22:1; Isa 59:2]
Hadi lini utanificha uso wako?
2Nitakuwa na wasiwasi rohoni mwangu hadi lini,
Nikihuzunika moyoni mchana kutwa?
Adui yangu atatukuka juu yangu hadi lini?
3Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie;[#Ezr 9:8; Zab 18:28; Lk 2:32; Ufu 21:23; Zab 76:5,6; Isa 37:36; Yer 51:39; Efe 5:14]
Uyatie nuru macho yangu,
Nisije nikalala usingizi wa mauti.
4Adui yangu asije akasema, Nimemshinda;
Watesi wangu wasifurahi ninapoondoshwa.
5Lakini mimi nimezitumainia fadhili zako;[#2 Nya 20:12]
Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.
6Naam, nitamwimbia BWANA,
Kwa kuwa amenitendea kwa ukarimu.