The chat will start when you send the first message.
1Chuo cha uzao wake Yesu Kristo, mwana wa Dawidi, mwana wa Aburahamu, ni hiki:[#1 Mambo 17:11; 1 Mose 22:18.]
2Aburahamu alimzaa Isaka, Isaka akamzaa Yakobo, Yakobo akamzaa Yuda na nduguze,[#1 Mose 21:3,12; 25:26; 29:35; 49:10.]
3Yuda na Tamari wakamzaa Peresi na Zera, Peresi akamzaa Hesiromu, Hesiromu akamzaa Ramu,[#1 Mose 38:29-30.]
4Ramu akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Nasoni, Nasoni akamzaa Salmoni.[#Ruti 4:18-22; 1 Mambo 3:10-19.]
5Salmoni na Rahabu wakamzaa Boazi, Boazi na Ruti wakamzaa Obedi, Obedi akamzaa Isai,[#Ruti 4:13-17.]
6Isai akamzaa mfalme Dawidi.[#2 Sam. 12:24.]
7Dawidi na mkewe Uria wakamzaa Salomo,[#1 Mambo 3:10-16.]
8Salomo akamzaa Rehabeamu, Rehabeamu akamzaa Abia, Abia akamzaa Asafu, Asafu akamzaa Yosafati, Yosafati akamzaa Yoramu, Yoramu akamzaa Uzia,
9Uzia akamzaa Yotamu, Yotamu akamzaa Ahazi, Ahazi akamzaa Hizikia,
10Hizikia akamzaa Manase, Manase akamzaa Amoni, Amoni akamzaa Yosia,
11Yosia akamzaa Yekonia na nduguze siku zile, walipohamishwa kwenda Babeli.
12Walipokwisha kuhamishwa kwenda Babeli, Yekonia akamzaa Saltieli, Saltieli akamzaa Zerubabeli,[#1 Mambo 3:17; Ezr. 3:2.]
13Zerubabeli akamzaa Abihudi, Abihudi akamzaa Eliakimu, Eliakimu akamzaa Azoro,
14Azoro akamzaa Sadoko, Sadoko akamzaa Ahimu, Ahimu akamzaa Elihudi,
15Elihudi akamzaa Elazari, Elazari akamzaa Matani, Matani akamzaa Yakobo,
16Yakobo akamzaa Yosefu, mumewe Maria aliyekuwa mama yake Yesu aitwaye Kristo.[#Mat. 27:17,22.]
17Basi, vizazi vyote tangu Aburahamu mpaka Dawidi ni vizazi 14; tangu Dawidi mpaka kuhamishwa kwenda Babeli ni vizazi 14, tena tangu kuhamishwa kwenda Babeli mpaka Kristo ni vizazi 14.
18Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi: Maria, mama yake, alionekana ana mimba kwa nguvu ya Roho Mtakatifu hapo, alipokuwa ameposwa na Yosefu, nao walikuwa hawajakaribiana.[#Luk. 1:35.]
19Yosefu, mchumba wake, alikuwa mwongofu, tena hakutaka kumwumbua, kwa hiyo alitaka kumwacha tu, watu wasijue.
20Alipokuwa akiyafikiri haya, mara malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto akisema: Yosefu, mwana wa Dawidi, usiogope kumwoa Maria, Mchumba wako, kwani kitakachozaliwa naye ni cha Roho Mtakatifu.[#Mat. 1:18.]
21Atazaa mtoto mwanamume, naye utamwita jina lake Yesu. Kwani yeye ndiye atakayewaokoa watu wake katika makosa yao.[#Luk. 1:31; 2:21; Tume. 4:12; Sh. 130:8.]
22Haya yote yalifanyika, lipate kutimia lililonenwa na Bwana kwa mfumbuaji:[#Yes. 7:14.]
23Tazama, mwanamwali atapata mimba, atazaa mtoto
mwanamume, nalo jina lake watamwita Imanueli, ni kwamba:
Mungu yuko nasi.*
24Yosefu alipoamka katika usingizi akatenda, kama malaika wa Bwana alivyomwagiza. Akamwoa mchumba wake,
25lakini hakumkaribia, mpaka alipomzaa mwanawe wa kwanza. Akamwita jina lake YESU.[#Luk. 2:7.]