The chat will start when you send the first message.
1Mvinyo ni mfyozaji, nacho kileo huleta makelele,
kila atokaye hapo na kupepesuka hakuerevuka.
2Tisho la mfalme ni ngurumo ya simba,
amkasirishaye hujikosea mwenyewe.
3Mtu ajitengaye penye ugomvi huheshimiwa,
lakini kila mjinga hukenua meno.
4Mvivu hataki kulima tangu hapo, kipupwe kinapoanza,
tena akitafuta vilaji mavunoni, haviko.
5Maji yenye lindi ni mashauri yaliyomo noyoni mwa mtu,
lakini mtu mtambuzi hujua kuyateka.
6Watu wengi hutangaza, ila mtu akizikuza huruma zake yeye,
lakini aonaye mtu mwenye welekevu wa kweli yuko nani?
7Aishikaye njia yake pasipo kukosa ni mwongofu,
wanawe wamfuatao nyuma ndio wenye shangwe.
8Mfalme akaaye katika kiti chake cha kukatia mashauri
huyatawanya kwa macho yake mabaya yote.
9Yuko nani awezaye kusema: Nimeung'aza moyo wangu?
Nimetakata, makosa yangu yamekwisha kuondoka?
10Vipimo vya namna mbili na pishi za namna mbili,
zote mbili humtapisha Bwana.
11Hata kijana hujulika kwa matendo yake,
kama kazi zake zinatakata, kama zinakwenda sawa.
12Sikio lisikialo na jicho lionalo,
Bwana ndiye ayatengenezaye yote mawili.
13Usiupende usingizi, usije kuwa mkosefu!
Yafumbue macho yako! Ndipo, utakaposhiba chakula.
14Mnunuzi husema: Ni kibaya, ni kibaya,
lakini akiisha kwenda zake hujichekea.
15Ingawa dhahabu ni lulu ziwe nyingi,
lakini kiko kitu kizipitacho, ndio midomo yenye ujuzi.
16Zichukue nguo zake yeye aliyejitoa kuwa dhamana ya mwingine,
kwa ajili yao walio wageni mnyang'anye yeye mali zake.
17Vilaji vilivyopatwa kwa udanganyifu mtu huviona kuwa vitamu,
lakini mwisho kinywa chake hujaa vijiwe vya changarawe.
18Mawazo yaliyopigiwa mashauri mema hufanikiwa,
ukipiga vita vipige na kuzitumia akili!
19Atembeaye na kusingizia hufunua mashauri ya njama,
naye afumbuaye midomo usifanye bia naye.
20Amwapizaye baba yake na mama yake,
taa yake huzimika katika giza lizidishalo.
21Ukianza kujipatia fungu la mali kwa kupokonya upesiupesi,
mwisho hazibarikiwi.
22Usiseme: Na nilipishe mabaya!
Ila mngojee Bwana! Ndiye atakayekusaidia.
23Vipimo viwili humtapisha Bwana,
nayo mizani ya kudanganyia haifai.
24Bwana ndiye anayeiendesha miguu ya mtu,
maana mtu anawezaje kuitambua njia yake?
25Mtu hujinasa kwa kujisemea tu: Hii mali ya Bwana,
na kuyafikiri halafu, aliyoyaapa.
26Mfalme mwerevu wa kweli huwapepeta wasiomcha Mungu,
akipitisha juu yao gari la kupuria.
27Roho ya mtu ni taa, aliyopewa na Bwana,
nayo huyachunguza yote yaliyomo tumboni.
28Upole na welekevu humlinda mfalme,
naye hukishikiza kiti chake cha kifalme kwa upole.
29Utukufu wa vijana ni nguvu zao,
nao urembo wa wazee ni mvi.
30Mavilio yenye vidonda humtakasa mtu, mabaya yamtoke,
ijapo mapigo yaingie mpaka tumboni ndani.