The chat will start when you send the first message.
1Basi manabii, Hagai nabii, na Zekaria mwana wa Ido, wakawafanyia unabii Wayahudi waliokuwako Yerusalemu na Yuda; waliwafanyia unabii kwa jina la Mungu wa Israeli.[#Hag 1:1; Zek 1:1]
2Ndipo akaondoka Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yosadaki, wakaanza kuijenga nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu; na pamoja nao walikuwa manabii wa Mungu, wakiwasaidia.[#Hag 1:12-15; Ezr 6:14; Mhu 12:11; Hag 2:4-9]
3Wakati ule ule Tatenai, Mkuu wa mkoa wa ng'ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzao, wakawajia, wakawaambia, Ni nani aliyewapa amri kuijenga nyumba hii, na kuumaliza ukuta huu?[#Ezr 6:6]
4Ndipo wakawauliza hivi, Majina ya watu wanaofanya ujenzi huu ni gani?
5Lakini jicho la Mungu lilikuwa likiwaelekea wazee wa Wayahudi, hao wasiwazuie hadi habari ile imfikie Dario, ndipo jawabu itakapopatikana kwa waraka.[#2 Nya 16:9; Ezr 7:6,28; Zab 33:18; Isa 41:10; 1 Pet 3:12]
6Hii ndiyo nakala ya waraka ambao; Tatenai, Mkuu wa mkoa wa ng'ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzake wa Kiajemi, waliokuwako huko ng'ambo ya Mto; walimtumia mfalme Dario.[#Ezr 4:9]
7Walimtumia ripoti; na maneno haya yakaandikwa ndani yake;