Ezra 7

Ezra 7

Kuwasili kwa Ezra na kazi yake

1Ikawa baada ya mambo hayo, wakati wa kutawala kwake Artashasta, mfalme wa Uajemi, Ezra, mwana wa Seraya, mwana wa Azaria, mwana wa Hilkia,[#Neh 2:1; 1 Nya 6:14]

2mwana wa Shalumu, mwana wa Sadoki, mwana wa Ahitubu,

3mwana wa Amaria, mwana wa Azaria, mwana wa Merayothi,

4mwana wa Zerahia, mwana wa Uzi, mwana wa Buki,

5mwana wa Abishua, mwana wa Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni, kuhani mkuu;

6huyo Ezra akakwea kutoka Babeli; naye alikuwa mwandishi mwepesi katika Sheria ya Musa, aliyokuwa ameitoa BWANA, Mungu wa Israeli; naye mfalme akamjalia matakwa yake yote, kama mkono wa BWANA, Mungu wake, ulivyokuwa pamoja naye.[#Mwa 32:28; Ezr 6:22; Neh 1:10,11]

7Nao wakakwea baadhi ya wana wa Israeli, na wa makuhani, na wa Walawi, na waimbaji, na mabawabu, na Wanethini, ili kwenda Yerusalemu, katika mwaka wa saba wa mfalme Artashasta.[#Ezr 8:1; 2:43]

8Naye Ezra akafika Yerusalemu mwezi wa tano katika mwaka wa saba wa huyo mfalme.

9Maana alianza kukwea kutoka Babeli siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, naye akafika Yerusalemu siku ya kwanza ya mwezi wa tano, kama mkono mwema wa Mungu wake ulivyokuwa pamoja naye.[#Neh 2:8]

10Kwa maana huyo Ezra alikuwa ameuelekeza moyo wake kuitafuta sheria ya BWANA, na kuitenda, na kufundisha maagizo na hukumu katika Israeli.[#1 Sam 7:3; 2 Nya 12:14; Zab 10:18; 119:45; Kum 33:10; Neh 8:1; Mal 2:7; 2 Tim 4:2]

Barua ya Artashasta kwa Ezra

11Basi hii ndiyo nakala ya barua, ambayo mfalme Artashasta alimpa Ezra, kuhani, mwandishi, mjuzi wa amri za BWANA, na sheria zake alizowapa Waisraeli.

27Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa baba zetu, aliyetia neno kama hilo katika moyo wa mfalme, kuipamba nyumba ya BWANA iliyoko Yerusalemu.[#1 Nya 29:10; Ezr 6:22; Flp 4:10; Neh 2:12; Mit 16:7; 2 Kor 8:16]

28Naye amenifikishia rehema zake mbele ya mfalme, na washauri wake, na mbele ya wakuu wote wa mfalme wenye mamlaka. Nami nikatiwa nguvu, kwa kadiri mkono wa BWANA, Mungu wangu, ulivyokuwa pamoja nami, nikawakusanya wakuu wote katika Israeli, ili wakwee pamoja nami.[#Ezr 9:9; Neh 1:11; Ezr 5:5]

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya