The chat will start when you send the first message.
1Sehemu waliopewa wana wa Yusufu ilianza kutoka mto wa Yordani hapo Yeriko, hapo penye maji ya Yeriko upande wa mashariki, maana, ni hiyo nyika, kukwea kutoka Yeriko kati ya hiyo nchi ya vilima mpaka Betheli;[#Hes 33:45]
2kisha ikatoka huko Betheli kwendelea Luzu, kisha ikaendelea hata kuufikia mpaka wa Waarki mpaka Atarothi;[#Mwa 28:19; Yos 18:13; Amu 1:26]
3kisha ikateremkia upande wa magharibi hadi kuufikia mpaka wa Wayafleti, hadi mpaka wa Beth-horoni ya chini, hadi kufikia Gezeri; na matokeo yake yalikuwa hapo baharini.[#Yos 18:13; 21:22; 2 Nya 8:5; 1 Nya 7:28; 1 Fal 9:15]
4Na wana wa Yusufu, Manase na Efraimu, walitwaa urithi wao.[#Yos 17:14]
5Na mpaka wa wana wa Efraimu kwa kufuata jamaa zao ulikuwa hivi; mpaka na urithi wao upande wa mashariki ulikuwa ni Ataroth-adari, hata Beth-horoni wa juu;[#Yos 18:13; 2 Nya 8:5]
6kisha mpaka ukatokea kwendelea upande wa magharibi huko Mikmeta upande wa kaskazini; kisha mpaka ukazunguka kwendea upande wa mashariki hata Taanath-shilo, kisha ukaendelea upande wa mashariki wa Yanoa;[#Yos 17:7]
7kisha uliteremka kutoka Yanoa hadi Atarothi, na Naara, kisha ukafika Yeriko, na kutokea hapo penye mto wa Yordani.[#1 Nya 7:28]
8Kutoka hapo Tapua mpaka ukaendelea upande wa magharibi hadi kijito cha Kana; na mwisho wake ulikuwa baharini. Huo ndio urithi wa hao wana wa Efraimu kwa kufuata jamaa zao;[#Yos 17:9; 19:28]
9pamoja na ile miji iliyotengwa kwa ajili ya wana wa Efraimu katikati ya urithi wa hao wana wa Manase, miji yote pamoja na vijiji vyake.
10Nao hawakuwatoa Wakanaani waliokuwa wakikaa Gezeri; lakini hao Wakanaani waliketi kati ya Efraimu, hata hivi leo, wakawa watumishi wa kufanya kazi za shokoa.[#Amu 1:29; Yos 15:63; 1 Fal 9:16,20,21; Mwa 9:25; Yos 17:12,13]