Yoshua 19

Yoshua 19

Nchi ya Simeoni

1Kisha sehemu ya pili ilitokea kwa ajili ya Simeoni, maana, kwa ajili ya hilo kabila la wana wa Simeoni, kwa kufuata jamaa zao; na urithi wao ulikuwa katikati ya urithi wa wana wa Yuda.[#Mwa 49:7]

2Miji waliyokuwa nayo katika urithi wao ni Beer-sheba, Sheba, Molada;[#1 Nya 4:28-33; Mwa 21:14,31; 26:33; Yos 15:28; Neh 11:26]

3Hasar-shuali, Bala, Esemu;

4Eltoladi, Bethuli, Horma;[#1 Nya 4:29,30]

5Siklagi, Beth-markabothi, Hasarsusa;

6Bethlebaothi na Sharuheni; miji kumi na mitatu, pamoja na vijiji vyake;

7Aini, Rimoni, Etheri na Ashani; miji minne, pamoja na vijiji vyake;

8tena vijiji vyote vilivyozunguka miji hiyo kotekote mpaka Baalath-beeri, Rama wa Kusini. Huo ndio urithi wa kabila la wana wa Simeoni kwa kuandama jamaa zao.

9Huo urithi wa hao wana wa Simeoni ulitoka katika fungu la wana wa Yuda; kwa maana hilo fungu la wana wa Yuda lilikuwa ni kubwa mno kwao; kwa hiyo wana wa Simeoni walikuwa na urithi katikati ya urithi wao.

Nchi za Zabuloni

10Kisha sehemu ya tatu ilitokea kwa ajili ya wana wa Zabuloni kwa kufuata jamaa zao; na mpaka wa urithi wao ulifikia hadi Saridi;

11kisha mpaka wao ukakwea kwendelea upande wa magharibi, hadi kufikia Marala, nao ukafikia hadi Dabeshethi; nao ukafikia kijito cha maji kilicho mkabala wa Yokneamu;[#Mwa 49:13; Kut 23:31; Hes 34:6,7; Yos 12:22; 1 Fal 4:12; 1 Nya 6:68]

12kisha ukazunguka kutoka Saridi kwendelea upande wa mashariki kwa kuelekea maawio ya jua hata kufikia mpaka wa Kisiloth-ubori; kisha ukatokea hata Daberathi, kisha ukakwea kwendelea Yafia;

13kutoka hapo ukaendelea kuelekea mashariki mpaka Gath-heferi, hadi kufikia Ethkasini; kisha ukatokea huko Rimoni ufikialo hadi Nea;

14kisha mpaka uliizunguka nchi hiyo kwa upande wa kaskazini hadi Hanathoni; kisha mwisho wake ulikuwa katika bonde la Iftaeli;

15Katathi, Nahalali, Shimroni, Idala na Bethlehemu; miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake.[#Yos 21:34; Amu 1:30; Yos 11:1; 12:20]

16Huu ndio urithi wa wana wa Zabuloni kwa kufuata jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake.[#Mdo 17:26]

Nchi ya Isakari

17Kisha sehemu ya nne ilitokea kwa ajili ya Isakari, maana, ni kwa ajili ya wana wa Isakari kwa kufuata jamaa zao.

18Na mpaka wao ulifikia Yezreeli, Kesulothi, Shunemu;[#Yos 15:16; Amu 6:33; 1 Fal 21:1,23; 2 Fal 8:29; 9:15,30; Hos 1:4,5; 1 Sam 28:4; 2 Fal 4:8]

19Hafaraimu, Shioni, Anaharathi;

20Rabithu, Kishioni, Ebesi;

21Remethi, Enganimu, Enhada, Bethpasesi;[#Yos 21:29]

22na mpaka ukafikia hadi Tabori, na Shahasuma na Beth-shemeshi; na mwisho wa mpaka wao ulikuwa katika mto wa Yordani; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.[#Amu 4:6; 1 Sam 10:3; 1 Nya 6:77; Zab 89:12; Yer 46:18]

23Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Isakari kwa kufuata jamaa zao; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.

Nchi ya Asheri

24Kisha sehemu ya tano ilitokea kwa ajili ya kabila la wana wa Asheri kwa kufuata jamaa zao.

25Na mpaka wao ulikuwa ni Helkathi, Hali, Beteni, Akishafu;[#2 Sam 2:16; 1 Nya 6:75]

26Alameleki, Amadi na Mishali; nao ukafika hadi Karmeli upande wa magharibi, tena ulifikia hadi Shihor-libnathi;[#1 Fal 18:19; 2 Fal 2:25; 4:25; Isa 35:2; Yer 46:18; Amo 1:2; 9:3; Mik 7:14]

27kisha ukazunguka kuelekea maawio ya jua mpaka Beth-dagoni, nao ukafikia hadi Zabuloni, tena mpaka bonde la Iftaeli upande wa kaskazini hadi Bethemeki na Neyeli; kisha ukatokea hadi Kabuli upande wa kushoto;[#1 Fal 9:13]

28na Ebroni, Rehobu, Hamoni, Kana, hadi kufikia Sidoni Kuu;[#Yn 2:1; Mwa 10:15,19; Yos 11:8; Amu 1:31; 10:12; Mdo 27:3]

29kisha mpaka ulizunguka kuelekea Rama, na mji wa Tiro ulio na boma; kisha mpaka ulizunguka kuelekea Hosa; na matokeo yake yalikuwa baharini katika nchi ya Akzibu;[#2 Sam 5:11; Mwa 38:5; Amu 1:31; Mik 1:14]

30na Uma pia, na Afeka, na Rehobu; miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake.

31Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Asheri kwa kufuata jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake.

Nchi ya Naftali

32Kisha sehemu ya sita ikatokea kwa ajili ya wana wa Naftali, maana, ni kwa ajili ya wana wa Naftali kwa kufuata jamaa zao.

33Na mpaka wao ulikuwa kutoka Helefu, tokea ule mwaloni ulio katika Saananimu, na Adami-nekebu, na Yabneeli, hadi kufikia Lakumu; na matokeo yake yalikuwa katika mto wa Yordani;

34tena mpaka ulizunguka kwendelea upande wa magharibi hadi Aznoth-tabori, tena kutoka hapo ukaendelea mpaka Hukoki; kisha ukafikia hadi Zabuloni upande wa kusini, tena ulifikia hadi Asheri upande wa magharibi, tena ulifikia hata Yuda hapo katika mto wa Yordani kwa upande wa kuelekea maawio ya jua.[#Kum 33:23]

35Na miji yenye boma ilikuwa ni hii, Sidimu, Seri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi;[#Mwa 10:18; Hes 13:21; 1 Fal 8:65; 2 Fal 14:25; Yer 39:5; Kum 3:17; Yos 11:2; 12:3; Mk 6:53; Lk 5:1]

36Adama, Rama Hazori;

37Kedeshi, Edrei, Enhasori;

38Ironi, Migdal-eli, Horemu, Bethanathi na Beth-shemeshi; miji kumi na tisa, pamoja na vijiji vyake.

39Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Naftali kwa kufuata jamaa zao; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.

Nchi ya Dani

40Kisha sehemu ya saba ilitokea kwa ajili ya kabila la wana wa Dani kwa kufuata jamaa zao.

41Na mpaka wa urithi wao ulikuwa ni Sora, Eshtaoli, Irishemeshi;[#Amu 13:2]

42Shaalabini, Aiyaloni, Ithla;[#Amu 1:35; 1 Fal 4:9]

43Eloni, Timna, Ekroni;

44Elteka, Gibethoni, Baalathi;

45Yehudi, Bene-beraki, Gath-rimoni;

46Meyarkoni na Rakoni, pamoja na huo mpaka uliokuwa mkabala wa Yafa.

47Kisha mpaka wa wana wa Dani ulitokea kuwapita wao; kwa kuwa hao wana wa Dani wakakwea na kupigana na Leshemu, na kuutwaa, na kuupiga kwa makali ya upanga, na kuumiliki, nao wakakaa humo, wakauita Dani, kwa kuliandama jina la huyo Dani mzee wao.[#Amu 18:27-29; 18:1; Mwa 49:17]

48Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Dani kwa kufuata jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake.[#Hes 26:54; Mdo 17:26]

Nchi ya Yoshua

49Basi walipomaliza kazi yao hiyo ya kuigawanya nchi iwe urithi kwa kufuata mipaka yake; wana wa Israeli kakampa Yoshua, mwana wa Nuni, urithi katikati yao;

50kulingana na ile amri ya BWANA wakampa mji alioutaka, maana, ni Timnath-sera katika nchi ya vilima ya Efraimu; naye akaujenga huo mji na kukaa mumo.[#Yos 24:30; 1 Nya 7:24]

51Hizi ndizo nchi, ambazo Eleazari kuhani, na Yoshua huyo mwana wa Nuni, pamoja na hao vichwa vya nyumba za mababa ya makabila ya Waisraeli, walizigawanya kwa njia ya kupiga kura, ziwe urithi, huko Shilo mbele ya BWANA, hapo mlangoni mwa hema ya kukutania. Basi hivyo wakamaliza kazi ya kuigawanya hiyo nchi.[#Hes 34:17; Yos 14:1; 18:1,10; Amu 21:19; Zab 78:58; Yer 7:12; 26:6]

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya