The chat will start when you send the first message.
1BWANA akanena na Musa katika jangwa la Sinai, hemani mwa kukutania, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, katika mwaka wa pili baada ya kutoka kwao nchi ya Misri, akamwambia,[#Hes 26:1-51; Kut 19:1; Law 27:34; Hes 10:12; Kut 25:22; Law 1:1]
2Fanyeni hesabu ya watu wote wa Israeli, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina ilivyo, kila mwanamume mmoja mmoja;[#Kut 30:12; 38:26; Hes 26:2-4,63,64; 1 Nya 21:2; 2 Sam 24:2]
3kuanzia aliye na umri wa miaka ishirini na zaidi, wote wawezao kutoka kwenda vitani katika Israeli; wewe na Haruni mtawahesabu kwa kufuata majeshi yao.
4Tena mwanamume mmoja wa kila kabila atakuwa pamoja nanyi; kila mmoja aliye kichwa cha nyumba ya baba zake.[#Hes 2:2; 1 Nya 27:1]
5Haya ndiyo majina ya wanaume watakaokusaidia; Wa Reubeni; Elisuri mwana wa Shedeuri.[#Mwa 29:32; Kut 1:2; Kum 33:6; Ufu 7:4]
6Wa Simeoni; Shelumieli mwana wa Suri-shadai.
7Wa Yuda; Nashoni mwana wa Aminadabu.[#Hes 7:12; 10:14; Rut 4:20; 1 Nya 2:10; Lk 3:32]
8Wa Isakari; Nethaneli mwana wa Suari.
9Wa Zabuloni; Eliabu mwana wa Heloni.
10Katika wana wa Yusufu; wa Efraimu, Elishama mwana wa Amihudi; na wa Manase; Gamalieli mwana wa Pedasuri.
11Wa Benyamini Abidani mwana wa Gideoni.
12Wa Dani; Ahiezeri mwana wa Amishadai.
13Wa Asheri; Pagieli mwana wa Okirani.
14Wa Gadi; Eliasafu mwana wa Deueli.[#Hes 2:14]
15Wa Naftali; Ahira mwana wa Enani.
16Hao ndio waliochaguliwa na mkutano, wakuu wa makabila ya baba zao; nao ndio vichwa vya wa wale maelfu ya Israeli.[#Mwa 6:4; Kut 18:21; Hes 7:2; 1 Nya 5:24; Amu 6:15; Kut 18:21; Kum 1:15]
17Basi Musa na Haruni wakawatwaa watu hao, wanaume waliotajwa majina yao;
18nao waliwakutanisha watu wote, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, nao wakaonesha ukoo wa vizazi vyao kwa kufuata jamaa zao, kwa nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, mmoja mmoja.[#Ezr 2:59; Neh 7:61; Ebr 7:3]
19Kama BWANA alivyomwagiza Musa, ndivyo alivyowahesabu huko katika jangwa la Sinai.[#Hes 26:1,2; 1 Nya 27:23,24; 2 Sam 24:1]
20Na wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kichwa kwa kichwa, kila mwanamume kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi wote walioweza kwenda vitani;
21wale waliohesabiwa katika kabila la Reubeni, walikuwa watu elfu arubaini na sita na mia tano (46,500) mmoja mmoja.
22Katika wana wa Simeoni, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, wale waliohesabiwa kama hesabu ya majina, kichwa kwa kichwa, kila mwanaume kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani;[#2 Sam 22:35; Zab 44:3; 60:12; 1 Kor 16:13; 2 Kor 3:5; Efe 6:12]
23wale waliohesabiwa katika kabila la Simeoni, walikuwa watu elfu hamsini na tisa na mia tatu (59,300).
24Katika wana wa Gadi, kwa kufuata vizazi vyao, jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani;[#Mwa 30:11; 49:19; Yos 4:12; Ufu 7:5]
25wale waliohesabiwa katika kabila la Gadi, walikuwa watu elfu arubaini na tano, mia sita na hamsini (45,650).
26Katika wana wa Yuda, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani;[#Mwa 29:35; 49:8-10; Zab 78:68; Mt 1:2; Ebr 7:14; Ufu 5:5]
27wale waliohesabiwa katika kabila la Yuda, walikuwa watu elfu sabini na nne na mia sita (74,600).
28Katika wana wa Isakari, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kwa hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani;
29wale waliohesabiwa katika kabila la Isakari, walikuwa watu elfu hamsini na nne na mia nne (54,400).
30Katika wana wa Zabuloni, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani;
31wale waliohesabiwa katika kabila la Zabuloni, walikuwa watu elfu hamsini na saba na mia nne (57,400).
32Katika wana wa Yusufu, maana katika wana wa Efraimu, vizazi vyao kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani,[#Mwa 30:24; 48:15,20; Zab 60:7; 78:67; Yer 7:15]
33wale waliohesabiwa katika kabila la Efraimu, walikuwa watu elfu arubaini na mia tano (40,500).
34Katika wana wa Manase, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani;
35wale waliohesabiwa katika kabila la Manase, walikuwa watu elfu thelathini na mbili na mia mbili (32,200).
36Katika wana wa Benyamini, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani;[#Mwa 35:16-18; 44:20; 49:27; Zab 68:27; Ufu 7:8]
37wale waliohesabiwa katika kabila la Benyamini, walikuwa watu elfu thelathini na tano na mia nne (35,400).
38Katika wana wa Dani, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani;[#Mwa 30:5,6; 49:16,17]
39wale waliohesabiwa katika kabila la Dani, walikuwa watu elfu sitini na mbili na mia saba (62,700).
40Katika wana wa Asheri, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani;
41wale waliohesabiwa katika kabila la Asheri, walikuwa watu elfu arubaini na moja na mia tano (41,500).
42Katika wana wa Naftali, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani;
43wale waliohesabiwa katika kabila la Naftali, walikuwa watu elfu hamsini na tatu na mia nne (53,400).
44Hao ndio waliohesabiwa, ambao Musa na Haruni na wale wakuu wa Israeli watu kumi na wawili waliwahesabu; walikuwa kila mmoja kwa ajili ya nyumba ya baba zake.[#Hes 26:64]
45Basi hao wote waliohesabiwa katika wana wa Israeli kwa kufuata nyumba za baba zao kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi; wote walioweza kwenda vitani katika Israeli;
46hao wote waliohesabiwa walikuwa ni wanaume elfu mia sita na tatu, mia tano na hamsini (603,550).[#Mwa 13:16; Kut 12:37; 38:26; Kum 10:22; Hes 26:51; 1 Fal 4:20]
47Lakini Walawi kwa kulifuata kabila la baba zao hawakuhesabiwa katika watu hao.[#Hes 2:33; 3:1; 26:57; 1 Nya 6:1; 21:6]
48Kwa kuwa BWANA alinena na Musa, na kumwambia,
49Hilo kabila la Lawi tu usilihesabu, wala usiitie hesabu yao katika wana wa Israeli;[#Hes 26:62]
50lakini uwaweke Walawi wawe juu ya maskani ya ushahidi, na juu ya vyombo vyake vyote, na juu ya vitu vyake vyote; wao wataichukua hiyo maskani, na vyombo vyake vyote; nao wataitumikia, na kupanga hema zao kwa kuizunguka maskani pande zote.[#Kut 31:18; 32:26; Hes 3:7,8,23; 4:15-33; #1:50 Kut 25:16: Kisha tia ndani ya sanduku huo ushuhuda nitakaokupa.]
51Tena hapo maskani itakapokwenda mbele, Walawi wataishusha; tena hapo maskani itakaposimamishwa, Walawi wataisimamisha; na mgeni atakayekaribia atauawa.[#Hes 10:17,21]
52Na wana wa Israeli watazipanga hema zao, kila mtu katika kambi yake mwenyewe, kila mtu hapo ilipo bendera yake mwenyewe, kama majeshi yao yalivyo.
53Lakini Walawi watapanga hema zao kuizunguka maskani ya ushahidi pande zote, ili zisiwe hasira juu ya mkutano wa wana wa Israeli; kisha Walawi wahudumu katika hiyo Hema Takatifu.[#Law 10:6; Hes 8:19; 16:46; 1 Sam 6:19; Hes 8:24; 1 Nya 23:32; 2 Nya 13:10]
54Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli; kama yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya.