The chat will start when you send the first message.
1Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
2Nena na wana wa Israeli, na kuwaambia, Mtakapoingia nchi yenu ya kukaa, niwapayo,[#Law 23:10]
3nanyi mwataka kumsogezea BWANA sadaka kwa moto, kwamba ni sadaka ya kuteketezwa, au dhabihu ya kuchinjwa, ili kuondoa nadhiri, au iwe sadaka ya hiari, au katika sikukuu zenu zilizoamriwa, ili kumfanyia BWANA harufu ipendezayo, katika ng'ombe, au katika kondoo;[#Kut 29:18,25,41; Law 1:2,3; 7:16; 23:8,12; Kum 16:10; Mwa 8:21; Kut 29:18; Law 1:9; Eze 20:41; 2 Kor 2:15; Efe 5:2; Flp 4:18]
4ndipo yeye atakayetoa matoleo yake na amtolee BWANA sadaka ya unga ya sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba uliochanganywa na robo ya hini ya mafuta;[#Law 2:1; 6:14; Isa 66:20; Kut 29:40; Law 14:10]
5na divai kwa sadaka ya kinywaji, robo ya hini, utaiandaa pamoja na sadaka ya kuteketezwa, au kwa dhabihu ya kuchinjwa, kwa ajili ya kila mwana-kondoo.[#Hes 28:7]
6Au kwa ajili ya kondoo dume, utaiandaa sadaka ya unga ya sehemu za kumi mbili za efa ya unga mwembamba uliochanganywa na sehemu ya tatu ya hini ya mafuta;
7na kwa sadaka ya kinywaji utasongeza sehemu ya tatu ya hini ya divai, kuwa harufu ya kupendeza kwa BWANA.
8Tena hapo utakapomwandaa ng'ombe dume kwa sadaka ya kuteketezwa, au kwa dhabihu ya kuchinjwa, kwa kuondoa nadhiri, au kwa sadaka za amani kwa BWANA;[#Law 7:11]
9ndipo utakapotoa, pamoja na huyo ng'ombe, sadaka ya unga ya sehemu za kumi tatu za efa ya unga mwembamba uliochanganywa na nusu ya hini ya mafuta.
10Tena utasongeza nusu ya hini ya divai kwa sadaka ya kinywaji, kwa sadaka iliyosongezwa kwa moto, ya harufu ya kupendeza kwa BWANA.
11Ndivyo itakavyofanywa kwa kila ng'ombe, au kwa kila kondoo dume, au kwa kila mwana-kondoo dume, au kila mwana-mbuzi.
12Kama idadi ilivyo ya hao mtakaowaandaa, ndivyo mtakavyofanya kwa kila mmoja, sawa na idadi yao.
13Wote ambao wamezaliwa kwenu watafanya hayo yote kwa kufuata mfano huo, katika kusongeza sadaka kwa moto, ya harufu ya kupendeza kwa BWANA.
14Tena ikiwa mgeni amekaa kwenu, au mtu yeyote aliye kati yenu katika vizazi vyenu, naye anataka kusongeza sadaka kwa moto, na harufu ya kupendeza kwa BWANA; kama ninyi mfanyavyo, na yeye atafanya vivyo hivyo.
15Katika huo mkutano, kutakuwa na amri moja kwenu ninyi na kwa mgeni akaaye pamoja nanyi; ni amri ya milele katika vizazi vyenu; kama ninyi mlivyo, na mgeni atakuwa vivyo hivyo mbele za BWANA.[#Law 24:22; Hes 9:14; Gal 3:28; Kol 3:11]
16Itakuwa sheria moja na amri moja kwenu ninyi na kwa mgeni akaaye nanyi.[#Law 24:22]
17Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
18Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapoingia nchi niwapelekayo,
19ndipo itakapokuwa ya kwamba kila mtakapokula katika chakula cha nchi hiyo, mtamsogezea BWANA sadaka ya kuinuliwa.[#Yos 5:11,12]
20Kutoka kwa unga wenu mtakaokanda kwanza wa chengachenga mtasongeza sadaka ya unga wa kuinuliwa uwe sadaka ya kuinuliwa; vile vile kama mfanyavyo sadaka ya kuinuliwa ya sakafu ya kupuchukulia nafaka, ndivyo mtakavyoiinua.[#Kut 23:19; Kum 26:2,10; Neh 10:37; Mit 3:9; Law 2:14; 23:10]
21Malimbuko ya unga wenu mtampa BWANA sadaka ya kuinuliwa, katika vizazi vyenu.
22Tena mtakapokosa, msiyashike maagizo hayo yote BWANA aliyomwambia Musa,[#Law 4:2; 1 Yoh 2:1]
23hayo yote BWANA aliyowaagiza kwa mkono wa Musa, tangu siku hiyo BWANA aliyoleta maagizo, na baadaye katika vizazi vyenu
24ndipo itakapokuwa, kama ni kosa lililofanywa pasipo kujua, wala mkutano haukuwa na fahamu, ndipo mkutano wote utasongeza ng'ombe dume mdogo mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa, kuwa harufu ya kupendeza kwa BWANA, pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya kinywaji, kama amri ilivyo, na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi.[#Law 4:13,23; Hes 28:15; Ezr 6:17; 8:35]
25Naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya mkutano wote wa wana wa Israeli, nao watasamehewa; maana, lilikuwa ni kosa, nao wamekwisha leta matoleo yao, sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto, na sadaka yao ya dhambi pia wameileta mbele za BWANA kwa ajili ya kosa lao;[#Law 4:20; Dan 9:24; Rum 5:11; Ebr 2:17; 10:10-12; 1 Yoh 1:7; 2:1,2]
26nao mkutano wote wa wana wa Israeli watasamehewa, na mgeni akaaye kati yao; maana, katika habari za hao wote jambo hilo lilitendeka pasipo kujua.
27Tena kama mtu mmoja akifanya dhambi pasipo kujua, ndipo atasongeza mbuzi mmoja wa kike wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya dhambi.[#Law 4:27-31; Zab 19:13; Lk 12:48]
28Naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya huyo mtu akosaye, atakapofanya dhambi pasipo kujua, mbele za BWANA, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake; naye atasamehewa.[#Law 4:35]
29Mtakuwa na sheria moja kwa huyo afanyaye neno lolote pasipo kujua, kwa huyo aliyezaliwa kwenu kati ya wana wa Israeli, na kwa mgeni akaaye kati yao.
30Lakini mtu afanyaye neno lolote kwa kusudi, kama ni mzalia, kama ni mgeni, huyo amtukana BWANA; na mtu huyo atatupiliwa mbali na watu wake.[#Kum 17:12; Zab 19:13; Rum 10:16; Ebr 10:26; 1 Pet 2:10]
31Kwa sababu amelidharau neno la BWANA, na kuyavunja maagizo yake; mtu huyo atakatiliwa mbali, uovu wake utakuwa juu yake.[#Law 26:15,43; 2 Sam 12:9; Mit 13:13; Isa 30:12; Ebr 10:28; Eze 18:20]
32Kisha wakati huo wana wa Israeli walipokuwako jangwani, wakamwona mtu mmoja akikusanya kuni siku ya Sabato.[#Kut 35:2,3]
33Hao waliomwona akikusanya kuni wakamleta kwa Musa na Haruni, na kwa mkutano wote.
34Nao wakamweka kifungoni, maana, lilikuwa halijasemwa atakalotendwa.[#Law 24:12]
35BWANA akamwambia Musa, Mtu huyo lazima atauawa; mkutano wote watampiga kwa mawe huko nje ya kambi.[#Kut 31:14,15; Gal 3:5; 1 Fal 21:13; Mdo 7:58]
36Basi mkutano wote wakampeleka nje ya kambi, nao wakampiga kwa mawe, akafa; kama BWANA alivyomwagiza Musa.
37Kisha BWANA akasema na Musa, na kumwambia,
38Nena na wana wa Israeli, na kuwaagiza ya kwamba wajifanyie vishada katika ncha za nguo zao, katika vizazi vyao, tena ya kwamba watie katika kila kishada cha kila ncha nyuzi za rangi ya buluu;[#Kum 22:12; Mt 9:20; 23:5; Lk 8:43,44]
39nacho kitakuwa kwenu ni kishada, ili mpate kukiangalia, na kuyakumbuka maagizo yote ya BWANA, na kuyafanya; tena ili msiende kutangatanga kufuata mioyo yenu wenyewe, na macho yenu wenyewe, ambayo mlikuwa mkiyaandama kwa uasherati hapo kwanza;[#Kum 29:19; Ayu 31:7; Yer 9:14; Eze 6:9; Law 26:15,16; Zab 73:27; 106:39; Hos 2:2; Yak 4:4]
40ili mpate kukumbuka na kuyafanya maagizo yangu yote, na kuwa watakatifu kwa Mungu wenu.[#Law 11:44,45; Mt 5:48; Rum 12:1; Kol 1:22; 1 The 5:8; 1 Pet 1:15]
41Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.