Zaburi 112

Zaburi 112

Baraka za mwenye haki

1Haleluya.

Heri mtu yule amchaye BWANA,

Apendezwaye sana na maagizo yake.

2Wazawa wake watakuwa hodari duniani;

Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa.

3Nyumbani mwake mna utajiri na mali,[#Mit 3:16; 15:6; Isa 33:6; Mt 6:33; 2 Kor 6:10]

Na haki yake yadumu milele.

4Nuru huwaangaza wenye adili gizani;

Ana fadhili na huruma na haki.

5Heri atendaye fadhili na kukopesha;[#Lk 6:35]

Atengenezaye mambo yake kwa haki.

6Kwa maana hataondoshwa kamwe;

Mwenye haki atakumbukwa milele.

7Hataogopa habari mbaya;

Moyo wake u imara ukimtumainia BWANA.

8Moyo wake umethibitika hataogopa,

Hata awaone watesi wake wameshindwa.

9Ametoa kwa ukarimu, na kuwapa maskini,[#Lk 11:41; Rum 12:13; Mdo 4:35; 20:35; 2 Kor 8:9; 9:9; 1 Tim 6:18]

Haki yake yakaa milele,

Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.

10Asiye haki ataona na kusikitika,[#Lk 13:28]

Atasaga meno yake na kuondoka,

Matumaini ya wasio haki hupotea.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya