Zaburi 130

Zaburi 130

Kusubiri wokovu wa Mungu

1Ee BWANA, toka vilindini nimekulilia.[#Omb 3:55; Yon 2:2]

2Bwana, uisikie sauti yangu.

Masikio yako na yaisikilize

Sauti ya dua zangu.

3BWANA, kama Wewe ungehesabu maovu,[#Zab 143:2; Yn 8:7-9; Rum 3:20]

Ee Bwana, nani angesimama?

4Lakini kwako kuna msamaha,[#2 The 1:6; Zab 37:2; Yer 17:6; Kut 3:4-7; Efe 1:7; 1 Fal 8:40; Yer 33:8,9; Ebr 12:28]

Ili Wewe uogopwe.

5Nimemngoja BWANA, roho yangu imengoja,[#Isa 26:8]

Na neno lake nimelitumainia.

6Nafsi yangu inamngoja Bwana,

Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi,

Naam, walinzi waingojao asubuhi.

7Ee Israeli, umtarajie BWANA;[#Isa 55:7]

Maana kwa BWANA kuna fadhili,

Na kwake kuna ukombozi mwingi.

8Yeye atamkomboa Israeli na maovu yake yote.[#Mt 1:21; Tit 2:14]

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya