Zaburi 134

Zaburi 134

Sifa ya usiku

1Njoni, enyi watumishi wote wa BWANA,[#Law 8:35; 1 Nya 9:33; Zab 130:6; Lk 2:37]

Mhimidini BWANA

Ninyi mnaohudumu usiku

Katika nyumba ya BWANA.

2Painulieni patakatifu mikono yenu,[#Zab 28:2; 1 Tim 2:8]

Na kumhimidi BWANA.

3BWANA akubariki toka Sayuni,[#Zab 124:8; 128:5]

Aliyeziumba mbingu na nchi.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya