The chat will start when you send the first message.
1Usihangaike kwa sababu ya watenda mabaya,
Usiwahusudu wafanyao ubatili.
2Maana kama majani watakatika mara,
Kama miche mibichi watanyauka.
3Umtumaini BWANA ukatende mema,
Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.
4Nawe ujifurahishe katika BWANA,[#Ayu 27:10; Wim 2:3; Isa 58:14; 1 Pet 1:8]
Naye atakutimizia haja za moyo wako.
5Umkabidhi BWANA njia yako,[#Mt 6:25; 1 Pet 5:7]
Pia umtumainie, naye atakutendea.
6Ataitokeza haki yako kama nuru,[#Mik 7:9]
Na hukumu yako kama jina la adhuhuri.
7Utulie mbele za BWANA,
Nawe umngojee kwa subira;
Usihangaike juu ya afanikiwaye katika njia yake,
Wala mtu apangaye maovu.
8Ukomeshe hasira, uache ghadhabu,[#Ayu 5:2; Zab 73:3; Mit 14:29; Efe 4:26; Yak 1:19]
Usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya.
9Maana watenda mabaya watakatiliwa mbali,
Bali wamngojao BWANA ndio watakaoirithi nchi.
10Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo,
Utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo.
11Bali wenye upole watairithi nchi,[#Mt 5:5]
Watajifurahisha kwa wingi wa amani.
12Asiye haki hunuia mabaya juu ya mwenye haki,
Na kumsagia meno yake.
13BWANA atamcheka,[#1 Sam 26:10]
Maana ameona kwamba siku yake inakuja.
14Wasio haki wamefuta upanga na kupinda uta,
Wamwangushe chini maskini na mhitaji,
Na kuwaua wenye mwenendo wa unyofu.
15Upanga wao utaingia mioyoni mwao wenyewe,
Na nyuta zao zitavunjika.
16Kidogo alicho nacho mwenye haki ni bora[#Mit 15:16; 1 Tim 6:6]
Kuliko wingi wa mali wa wasio haki wengi.
17Maana mikono ya wasio haki itavunjika,
Bali BWANA huwategemeza wenye haki.
18BWANA huwatunza waaminifu,[#Zab 1:6; Isa 60:21]
Na urithi wao utakuwa wa milele.
19Hawataaibika wakati wa ubaya,[#Ayu 5:20]
Na siku za njaa watashiba.
20Bali wasio haki watapotea,
Nao wamchukiao BWANA watatoweka,
Kama uzuri wa mashamba,
Kama moshi watatoweka.
21Asiye haki hukopa wala halipi,
Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu.
22Maana waliobarikiwa na BWANA watairithi nchi,[#Mit 3:33]
Nao waliolaaniwa naye watakatiliwa mbali.
23Hatua za mtu mwema huimarishwa na BWANA,[#Zab 121:3; Mit 16:9]
Naye huipenda njia yake.
24Ajapojikwaa hataanguka chini,[#Mik 7:8; 2 Kor 4:9]
Maana BWANA humshika mkono na kumtegemeza.
25Nilikuwa kijana na sasa ni mzee,
Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa
Wala mzawa wake akiomba chakula.
26Mchana kutwa hufadhili na kukopesha,
Na mzao wake hubarikiwa.
27Jiepushe na uovu, utende mema,
Na kukaa hata milele.
28Kwa kuwa BWANA hupenda haki,[#Zab 11:7]
Wala hawaachi watauwa wake.
Wao hulindwa milele,
Bali mzawa wa wasio haki ataharibiwa.
29Wenye haki watairithi nchi,
Nao watakaa humo milele.
30Kinywa chake mwenye haki hunena hekima,
Na ulimi wake husema hukumu.
31Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake.
Hatua zake hazitelezi.
32Mtu asiye haki humvizia mwenye haki,
Na kutafuta jinsi ya kumwua.
33BWANA hatamwacha mkononi mwake,[#Zab 109:31]
Wala hatamwacha alaumiwe atakapohukumiwa.
34Wewe umngoje BWANA,
Uishike njia yake,
Naye atakutukuza uirithi nchi,
Utawaona Wasio haki wakiangamizwa.
35Nimemwona mtu asiye haki mkali sana,
Akijieneza kama mwerezi wa Lebanoni.
36Nikapita na kumbe! Hayuko,
Nikamtafuta wala hakuonekana.
37Umwangalie sana mtu mkamilifu,[#Ayu 1:1; Isa 32:17; Lk 2:25-30; Mdo 7:59,60; 1 The 4:17; 2 Tim 4:6-8; 2 Pet 1:14]
Umtazame mtu mnyofu,
Maana mwisho wake mtu huyo ni amani.
38Wakosaji wataangamizwa pamoja,
Wasio haki mwisho wao wataharibiwa.
39Na wokovu wa wenye haki una BWANA;[#Zab 3:8; Isa 12:2; Yon 2:8]
Yeye ni ngome yao wakati wa taabu.
40Naye BWANA huwasaidia na kuwaopoa;[#1 Nya 5:20; Dan 3:17]
Huwaopoa kutoka kwa wasio haki na kuwaponya;
Kwa kuwa wamemtumaini Yeye.