The chat will start when you send the first message.
1Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu,
Kizazi baada ya kizazi.
2Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia,[#Ayu 38:4-6; Mit 8:25]
Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.
3Wamrudisha mtu mavumbini,[#Mwa 3:19; Mhu 12:7]
usemapo, Rudini, enyi wanadamu.
4Maana miaka elfu machoni pako[#Ebr 13:8; 2 Pet 3:8]
Ni kama siku ya jana ikiisha kupita,
Na kama kesha la usiku.
5Wawafutilia wanadamu mbali kama ndoto,[#Isa 40:6]
wao ni kama majani yameayo asubuhi.
6Asubuhi yachipuka na kumea,[#Ayu 14:2; Zab 92:7]
Jioni yakatika na kukauka.
7Maana tumeangamia kwa hasira yako,
Na kwa ghadhabu yako tumezidiwa.
8Umeyaweka maovu yetu mbele zako,[#Zab 50:21; Yer 16:17; Zab 19:12; Mit 5:21; Mhu 12:14; Rum 2:16; 1 Kor 4:5; Ebr 4:12,13]
Dhambi zetu za siri katika mwanga wa uso wako.
9Maana kwa hasira yako maisha yetu yanapita punde,
Maisha yetu yanaisha kama kite.
10Miaka ya maisha yetu ni sabini,
Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini;
Tena kiburi chake ni taabu na ubatili,
Maana wakati unapita upesi nasi kutokomea punde.
11Ni nani aujuaye uweza wa hasira yako?
Na ghadhabu yako inayolingana na kicho chako?
12Basi, utufundishe kuzihesabu siku zetu,[#Zab 39:4]
Tujipatie moyo wa hekima.
13Urudi, Ee BWANA utakasirika hadi lini?[#Kum 32:36]
Wahurumie watumishi wako.
14Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako,
Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote.
15Utufurahishe kwa kadiri ya siku ulizotutesa,
Miaka sawa na ile tuliyopatwa na maovu.
16Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako,[#Zab 44:1; Hab 3:2]
Na utukufu wako kwa watoto wao.
17Na fadhili za BWANA, Mungu wetu, ziwe juu yetu,[#Isa 26:12; 2 The 2:16,17]
Na kazi ya mikono yetu uifanye thabiti,
Naam, kazi ya mikono yetu uifanikishe.