Wagalatia 6

Wagalatia 6

1NDUGU, mtu ajapogbafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrudini mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako nsijaribiwe wewe mwenyewe.

2Mchukuliane mizigo mkaitimize hivyo sharia ya Kristo.

3Maana mtu akijiona kuwa kitu, nae si kitu, ajidanganya nafsi yake.

4Lakini killa mtu aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakuwa na sababu ya kujisifu kwa nafsi yake tu, wala si kwa kujilinganislia na mwenzake.

5Maana killa mtu atachukua mzigo wake mwenyewe.

6Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi wake katika mema yote.

7Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

8Maana yeye apandae kwa mwili wake, katika mwili atavuna uharibifu; bali yeye apandae kwa Roho, katika Roho atavima uzima wa milele.

9Na tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia.

10Tuwapo na nafasi na tuwatendee watu wote mema; khassa watu walio wa nyumba ya imani.

11Tazameni kwa harufi gani kubwa nimewaandikieni kwa mkono wangu mimi mwenyewe.

12Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mwili, ndio wanaokushurutisheni kutahiriwa: wasiudhiwe tu kwa ajili ya msalaba wa Kristo.

13Kwa maana hatta wao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sharia; bali wanataka ninyi mtahiriwe, wapate kujisifia miili yenu.

14Lakini mimi, hasha nisijisifie kitu illa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.

15Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya.

16Na wote watakaoiendea kanuni hii, amani kwao na rehema, naam, kwa Israeli wa Mungu.

17Tangu sasa mtu asinitie taabu; kwa maana ninachiukua mwilini mwangu chapa zake Yesu.

18Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja na roho zenu. Amin.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania