Waebrania 10

Waebrania 10

1BASSI kwa kuwa torati ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo, kwa dhahihu zile zile wanazozitoa killa mwaka daima, hawawezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.

2Kama wangeweza, wangeacha kuzitoa; kwa maana waabuduo, walipokwisha kusatishwa kwa marra moja, wasingejiona tena kuwa na dhamhi?

3Lakini katika hizo liko kumbukumbu la dhambi killa mwaka.

4Maana haiyumkini damu ya mafahali na mbuzi iondoe dhambi.

5Kwa biyo ajapo ulimwenguni, anena, Dhambi na toleo hukutaka, lakini mwili uliniwekea tayari:

6Kafara na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo:

7Ndipo nilisema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) niyafanye mapenzi yako, Mungu.

8Hapo juu anenapo, Dhabihu na matoleo na kafara na sadaka za dhamhi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo ilivyoamuru torati),

9ndipo alinena, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, illi kusudi alisimamishe la pili.

10Katika mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo marra moja.

11Na killa kuhani husimama killa siku akifanya ibada, akitoa dhabihu zilezile marra nyingi; nazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi.

12Lakini huyu, alipokwisha kutoa dhabihu nioja kwa dhambi, idumuyo hatta milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu;

13akingojea hatta adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake.

14Maana kwa toleo moja amewakamilisha hatta milele wanaotakaswa.

15Na Roho Mtakatifu yatushuhudia; kwa maana, baada ya kunena,

16Hili ni agano nitakalowapa baada ya siku zile, anna Bwana, Nitatia sharia zangu mioyoni mwao, na katika akili zao nitaziandika; ndipo anenapo.

17Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa.

18Bassi ondoleo la baya lilipo, hapana toleo tena kwa dhambi.

19Bassi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu,

20njia aliyotuanzia mpya, hayi, ipenyayo katika pazia, yaani mwili wake;

21na Kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu;

22tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa mwili kwa maji safi.

23Tulishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni amini;

24tukaangaliane kiasi cha kusukumana katika upendo na kazi nzuri;

25tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tukionyana; na tukizidi, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.

26Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;

27bali kuitazamia hukumu kwenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.

28Mtu aliyeidharau sharia ya Musa, alikufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.

29Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa nayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho ya neema?

30Maana twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake.

31Ni jambo la kutisba kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hayi.

32Lakini zikumbukeni siku za kwanza, ambazo, mlipokwisha kutiwa nuru, mlistahimili mashindano makubwa ya maumivu;

33pindi mlipotwezwa kwa mashutumu na mateso, na pindi mliposhirikiana na wale waliotendewa hayo.

34Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika mafungo, mkakubali kwa furaba kunyangʼauywa mali zenu, mkijua nafsini mwenu kwamba mna mali mbinguni iliyo njema zaidi, idumnyo.

35Bassi msiutupe njasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu.

36Maana mnahitaji uvumilivu, illi mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu muipate abadi.

37Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajae atakuja, wala hatakawia.

38Lakini mwenye haki ataishi kwa imani; nae akisitasita, roho yangu haina furaha nae.

39Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali miongoni mwao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania