The chat will start when you send the first message.
1BASSI, katika hayo tuuayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunae kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha ukuu mbinguni,
2mkhudumu wa patakatifu, na wa khema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwana Adamu.
3Maana killa kuhani mkuu awekwa illi atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu nae awe na kitu akitoe.
4Kama angekuwa juu ya inchi, asingekuwa kuliani; maana wapo watoapo sadaka kama iagizavyo sharia;
5watumikao kwa mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile khema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.
6Lakini sasa amepata khuduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mtengenezaji wa agano lililo bora, lililoamriwa kwa ahadi zilizo bora na kuzitegemea.
7Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili.
8Maana, awalaumupo, asema, Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya; halitakuwa kama agano lile nililofanyana na baba zao, katika siku ile nilipowashika mikono yao uiwatoe katika inchi ya Misri.
9Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, mimi nami sikuwaangalia, asema Bwana.
10Maana hili ndilo agano nitakalofanyana na nyumba ya Israeli baada ya siku zile, asema Bwana; nitatia sharia zangu katika nia zao, na katika mioyo yao nitaziandika; nami mtakuwa Mungu kwao, nao watakuwa watu waugu.
11Nao hawatafundishana killa mtu na jirani yake, na killa mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; kwa maana wote watunijua, tangu mdogo wao hatta mkubwa wao.
12Kwa sababu nitawasamehe dhumlumu zao, na dhambi zao sitazikumbuka tena.
13Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikukuu na kuchakaa ni karibu na kutoweka.