The chat will start when you send the first message.
1BASSI ikiwako faraja iliyo yote katika Kristo, yakiwako ma, tulizo yo yote ya mapenzi, ikiwako huruma yo yote na rehema,
2ijalizeni furaha yangu, illi mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja.
3Msitende neno lo lote kwa kushindana na kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, killa mtu na amhesabu mwenziwe kuwa hora kuliko nafsi yake;
4killa mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, hali killa mtu mamho ya wengine.
5Maana mwe na nia lili ndani yenu iliyokuwamo na ndani ya Yesu Kristo;
6yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, nae hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa kitu cha kushikamana nacho,
7hali alijifanya hana utukufu, akitwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wana Adamu;
8tena, alipoonekana ana umho kama mwana Adamu, alijidhili, akawa mtii hatta mauti, nayo mauti ya msalaba.
9Kwa hiyo tena Mungu akamtukuza mno, akamkarimia Jina lile lipitalo killa jina;
10illi kwa jina la Yesu killa goti likunjwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya inchi;
11killa ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
12Bassi, wapendwa, kama vile mlivyotii siku zote, si wakati mimi nilipokuwapo, bali sasa zaidi mimi nisipokuwapo, utimizeni wokofu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka;
13kwa maana ni Mungu atendae ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa ajili ya kusudi lake jema.
14Yatendeni mambo yote pasipo manungʼuniko na mashindano,
15mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala ndanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, na kilichopotoka; kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu, mkishika neno la uzima;
16nipate sababu ya kujisifu katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio burre wala sikujitaabisha burre.
17Naam, hatta nikimiminwa juu ya dhabihu na khuduma ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote.
18Nanyi vivyo hivyo furahini, tena furahini pamoja nami.
19Walakini natmnaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwemi karibu, nifarijiwe na mimi, nikiijua hali yenu.
20Maana sina mtu mwingine mwenye nia moja nami, atakaeangalia hali yenu kweli kweli.
21Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Yesu Kristo.
22Maana mwajua ya kuwa ametumika pamoja nami kwa ajili ya Injili, kama mwana na baba yake.
23Bassi, natumaini kumtuma huyu marra nitakapojua yatakayonipata.
24Maana naamini katika Bwana ya kuwa nitakuja na mimi mwenyewe karibu.
25Lakini naliona imenilazimu kumtuma Epafrodito, ndugu yangu, mtendaji wa kazi pamoja nami, askari pamoja nami; tena ni mtume wenu na mkhudumu wa muhitaji yangu.
26Kwa kuwa alikuwa na shanku kwenu ninyi nyote, akahuzunika sana, kwa sababu mlisikia ya kwamba alikuwa hawezi.
27Kwa maanu alikuwa hawezi kweli kweli, karibu na kufa; lakini Mungu alimhurumia; wala si yeye peke yake, illa na mimi pia: nisiwe na huzuni juu ya huzuni.
28Nikafanya hidii uyiugi zaidi kumtuma tena, nami nikapunguziwe huzuni yangu.
29Mpokeeni, bassi, katika Bwana, kwa furaha yote, mkawahesabu watu kama huyu kuwa watu wa kuheshimiwa.
30Maana kwa ajili ya kazi ya Kristo alikaribia kufa, asiutunze uhayi wake; illi kusudi ayatimize yaliyopungua katika khuduma yenu kwangu.