The chat will start when you send the first message.
1Ee Mwenyezi-Mungu, Bwana wetu,
kweli jina lako latukuka duniani kote!
Utukufu wako waenea mpaka juu ya mbingu!
2Kwa sifa za watoto wadogo na wanyonyao,
umejiwekea ngome dhidi ya adui zako,
uwakomeshe waasi na wapinzani wako.
3Nikiangalia mbingu, kazi ya vidole vyako,
mwezi na nyota ulizozisimika huko,
4mtu ni nini, ee Mungu, hata umfikirie,[#Taz Zab 144:3; Ebr 2:6-8]
binadamu ni nini hata umjali?
5Umemfanya awe karibu kama Mungu,
umemvika fahari na heshima.
6Ulimpa madaraka juu ya kazi zako zote;[#Taz 1Kor 15:27; Efe 1:22; Ebr 2:8]
uliviweka viumbe vyote chini ya mamlaka yake:
7Kondoo, ng'ombe, na wanyama wa porini;
8ndege, samaki, na viumbe vyote vya baharini.
9Ee Mwenyezi-Mungu, Bwana wetu,
kweli jina lako latukuka duniani kote!