The chat will start when you send the first message.
2Abrahamu akamzaa Isaka,
Isaka akamzaa Yakobo,
Yakobo akawazaa Yuda na ndugu zake,
3Yuda akawazaa Peresi na Zera, ambao mama yao alikuwa Tamari,
Peresi akamzaa Esromu,
Esromu akamzaa Aramu,
4Aramu akamzaa Aminadabu,
Aminadabu akamzaa Nashoni,
Nashoni akamzaa Salmoni,
5Salmoni akamzaa Boazi, na mama yake Boazi alikuwa Rahabu,
Boazi akamzaa Obedi, ambaye mama yake alikuwa Ruthu,
Obedi akamzaa Yese,
6Yese akamzaa Daudi, aliyekuwa mfalme.
Daudi akamzaa Sulemani, ambaye mama yake ni yule aliyekuwa mke wa Uria.
7Sulemani akamzaa Rehoboamu,
Rehoboamu akamzaa Abiya,
Abiya akamzaa Asa,
8Asa akamzaa Yehoshafati,
Yehoshafati akamzaa Yoramu,
Yoramu akamzaa Uzia,
9Uzia akamzaa Yothamu,
Yothamu akamzaa Ahazi,
Ahazi akamzaa Hezekia,
10Hezekia akamzaa Manase,
Manase akamzaa Amoni,
Amoni akamzaa Yosia,
11wakati wa uhamisho wa Babeli, Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake.
Yekonia alimzaa Shealtieli,
Shealtieli akamzaa Zerubabeli,
13Zerubabeli akamzaa Abihudi,
Abihudi akamzaa Eliakimu,
Eliakimu akamzaa Azori,
14Azori akamzaa Sadoki,
Sadoki akamzaa Akimu,
Akimu akamzaa Eliudi,
15Eliudi akamzaa Eleazari,
Eleazari akamzaa Matani,
Matani akamzaa Yakobo,
16naye Yakobo akamzaa Yusufu, aliyekuwa mumewe Mariamu, mama yake Yesu, aitwaye Kristo.[#1:16 maana yake Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.]
18Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi: Mariamu mama yake alikuwa ameposwa na Yusufu, lakini kabla hawajakutana kimwili, Mariamu alionekana kuwa na mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
19Kwa kuwa Yusufu, mwanaume aliyekuwa amemposa alikuwa mtu mwadilifu, hakutaka kumwaibisha Mariamu hadharani, hivyo basi alikusudia kumwacha kwa siri.
20Lakini alipokuwa akifikiri kufanya jambo hili, malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto na kusema, “Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
21Naye atamzaa mwana, nawe utamwita jina Yesu, kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.”[#1:21 ni kwa Kiyunani, na kwa Kiebrania ni Yoshua au Yeshua ; maana yake Yehova ni wokovu.]
22Haya yote yalitukia ili litimie lile Bwana alilonena kupitia nabii, aliposema:
23“Tazama, bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, nao watamwita jina Imanueli” (maana yake, “Mungu pamoja nasi”).[#1:23 Isa 7:14]
24Yusufu alipoamka kutoka usingizini, akafanya jinsi alivyoagizwa na malaika wa Bwana, akamchukua Mariamu kuwa mke wake.
25Lakini hawakukutana kimwili hadi Mariamu alipojifungua mwanawe; akamwita jina Yesu.[#1:25 tafsiri zingine husema kifungua mimba]