Hesabu 1

Hesabu 1

Watu wahesabiwa kwa mara ya kwanza

1Bwana alisema na Musa katika Jangwa la Sinai, katika Hema la Kukutania, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, katika mwaka wa pili baada ya Waisraeli kutoka nchi ya Misri. Akamwambia,

2“Hesabu watu wa jumuiya yote ya Waisraeli kwa kufuata koo zao na jamaa zao, ukiorodhesha kila mwanaume kwa jina lake, mmoja mmoja.

3Wewe na Haruni mtawahesabu kwa migawanyo yao wanaume wote katika Israeli wenye miaka ishirini na kuendelea wanaoweza kutumika katika jeshi.

4Mwanaume mmoja kutoka kila kabila, kila aliye kiongozi wa jamaa yake, atawasaidia.

“kutoka Reubeni, ni Elisuri mwana wa Shedeuri;

6kutoka Simeoni, ni Shelumieli mwana wa Surishadai;

7kutoka Yuda, ni Nashoni mwana wa Aminadabu;

8kutoka Isakari, ni Nethaneli mwana wa Suari;

9kutoka Zabuloni, ni Eliabu mwana wa Heloni;

10kutoka wana wa Yusufu:

11kutoka Benyamini, ni Abidani mwana wa Gideoni;

12kutoka Dani, ni Ahiezeri mwana wa Amishadai;

13kutoka Asheri, ni Pagieli mwana wa Okrani;

14kutoka Gadi, ni Eliasafu mwana wa Deueli;

15kutoka Naftali, ni Ahira mwana wa Enani.”

17Musa na Haruni wakawachukua wanaume hao waliokuwa wamepewa majina yao,

18wakaita jumuiya yote pamoja katika siku ya kwanza ya mwezi wa pili. Watu wakaonesha nasaba zao kwa koo zao na jamaa zao, nao wanaume waliokuwa na miaka ishirini au zaidi waliorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja,

19kama Bwana alivyomwagiza Musa. Hivyo aliwahesabu katika Jangwa la Sinai:

20Kutoka wazao wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Israeli:

22Kutoka wazao wa Simeoni:

24Kutoka wazao wa Gadi:

26Kutoka wazao wa Yuda:

28Kutoka wazao wa Isakari:

30Kutoka wazao wa Zabuloni:

Kutoka wazao wa Efraimu:

34Kutoka wazao wa Manase:

36Kutoka wazao wa Benyamini:

38Kutoka wazao wa Dani:

40Kutoka wazao wa Asheri:

42Kutoka wazao wa Naftali:

47Hata hivyo, jamaa ya kabila la Lawi hawakuhesabiwa pamoja na wengine.

48Bwana alikuwa amemwambia Musa:

49“Kamwe usihesabu kabila la Lawi wala kuwaweka pamoja katika hesabu ya Waisraeli wengine.

50Badala yake, waweke Walawi kuwa viongozi wa Maskani ya Ushuhuda, juu ya samani zake na kila kitu kilicho ndani yake. Wao watabeba Maskani na samani zake zote; wataitunza na kupiga kambi kuizunguka.

51Wakati wowote Maskani inapohamishwa, Walawi wataifungua, na wakati wowote Maskani inapotakiwa kusimamishwa, Walawi watafanya kazi hiyo. Mtu yeyote mwingine ambaye atasogea karibu nayo atauawa.

52Waisraeli watapiga mahema yao kwa makundi makundi, kila mwanaume katika kambi yake mwenyewe chini ya bendera yake.

53Hata hivyo, Walawi watapiga mahema yao kuzunguka Maskani ya Ushuhuda ili ghadhabu isiipate jumuiya ya Waisraeli. Walawi watawajibika kwa utunzaji wa Maskani ya Ushuhuda.”

54Waisraeli walifanya haya yote kama Bwana alivyomwamuru Musa.

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.