The chat will start when you send the first message.
1Msifuni Mwenyezi Mungu, ninyi nyote watumishi wa Mwenyezi Mungu,
ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya Mwenyezi Mungu.
2Inueni mikono yenu katika patakatifu
na kumsifu Mwenyezi Mungu.
3Naye Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na dunia,
awabariki kutoka Sayuni.