The chat will start when you send the first message.
1Mpumbavu anasema moyoni mwake,
“Hakuna Mungu.”
Wamepotoka, matendo yao ni maovu kabisa;
hakuna hata mmoja atendaye mema.
2Bwana anawachungulia wanadamu
kutoka mbinguni
aone kama kuna mwenye hekima,
yeyote anayemtafuta Mungu.
3Wote wamepotoka,
wote wameoza pamoja;
hakuna atendaye mema,
naam, hakuna hata mmoja!
4Je, watendao maovu kamwe hawatajifunza:
wale ambao huwala watu wangu
kama watu walavyo mkate,
hao ambao hawamwiti Bwana ?
5Wako hapo, wameingiwa na hofu kuu,
maana Mungu yupo pamoja na wenye haki.
6Ninyi watenda maovu mnakwamisha mipango ya maskini,
bali Bwana ndiye kimbilio lao.
7Laiti wokovu wa Israeli
ungekuja kutoka Sayuni!
Bwana anaporejesha
wafungwa wa watu wake,
Yakobo na ashangilie,
Israeli na afurahi!