The chat will start when you send the first message.
1Ee Bwana , tazama adui zangu walivyo wengi!
Ni wengi kiasi gani wanaoinuka dhidi yangu!
2Wengi wanasema juu yangu,
“Mungu hatamwokoa.”
3Lakini wewe, Ee Bwana , ni ngao yangu pande zote;
umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu.
4Ninamlilia Bwana kwa sauti kuu,
naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu.
5Ninajilaza na kupata usingizi;
naamka tena, kwa maana Bwana hunitegemeza.
6Sitaogopa makumi elfu ya adui,
wanaojipanga dhidi yangu kila upande.
7Ee Bwana , amka!
Niokoe, Ee Mungu wangu!
Wapige adui zangu wote kwenye taya,
vunja meno ya waovu.
8Kwa maana wokovu watoka kwa Bwana .
Baraka yako na iwe juu ya watu wako.